Tanzia: Baba mzazi wa Fid Q afariki Dunia

Tanzia: Baba mzazi wa Fid Q afariki Dunia.

Mwanamuziki wa Hiphop nchini Fareed Kubanda ‘Fid Q’ amefiwa na baba yake mzazi, Mzee Kubanda.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, @therelfidq ameandika “Ninasikitika kuwataarifu ya kwamba.. mzee wangu, baba yangu, Mzee Kubanda ametangulia mbele ya haki,”

Fid Q ameeleza kuwa mazishi ya babaye yatafanyika kesho kijijini kwake Nasa mkoani Mwanza.“Inna lillah wainna ilaih raajiuun (Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake tutarejea).” Ameandika Msanii huyo.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!