TUKIO: Aliyefariki mwaka 2020 aonekana akiwa hai 2024
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Bugumba Misalaba anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 Mkazi wa Mtaa wa Nyakato Kata ya Nyanguku Wilaya na Mkoa wa Geita aliyefariki kwa kugongwa na gari Wilayani humo September 07, 2020 ameonekana akitembea Mtaani mwaka huu jambo lililozua taharuki kwa Wakazi wa Mtaa huo.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Cornel Magembe amesema January 01, 2024 Mama huyo ameonekana jambo ambalo liliwafanya Walinzi waliokuwa wakilinda katika maeneo aliyoonekana kutoa taarifa Ofisi ya Serikali ya Mtaa.
“Tuliamini kwamba alifariki na kwakweli heshima zote na taratibu zote za Mtu aliyefariki zilifanyika na zilifanyika katika Kijiji hiki lakini kwa mshangao mkubwa January 01,2024 usiku saa mbili baadhi ya Watu ambao walikuwa wanafanya kazi ya ulinzi hapa walimuona Mwanamke huyu”
Magembe amewaonya Wananchi kwamba wasijaribu kuchukua sheria Mkononi kwenda kumdhuru Mwanamke huyo au Familia yake kwani Serikali itawachukulia hatua kali za kisheria.
Via: MillardAyoUPDATES
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!