Ujue Ute wa Ukeni rangi zake pamoja na Maana Zake

Ujue Ute wa Ukeni rangi zake pamoja na Maana Zake

Ute wa ukeni ni majimaji yanayotengenezwa na tezi ndogo ndani ya uke na shingo ya kizazi. Majimaji haya huvuja kutoka ukeni kila siku ili kuondoa seli za zamani na uchafu ukeni, kudumisha uke na njia ya uzazi kuwa safi na yenye afya. Ute huu hutofautiana kulingana na rangi, uzito, harufu na hata mtindo wake wa utokaji. Ute huu pia unaweza kuwa na msaada kukuwezesha kujua ishara nyingi ikiwemo siku za uchavushwaji, uwepo wa magonjwa na mengineyo, hivyo katika makala hii itaangalizia aina za ute, ishara gani zinamaanisha kwako kama mwanamke na ni vitu gani vya msingi kuzingatia au ni lini utahitaji msaada wa kitabibu.

Madoa kwenye nguo za ndani?

Kutokwa na ute sehemu za haja ndogo ni jambo la kawaida kabisa kwa wanawake waliopevuka. Ute huu wakati ukiwa unatoka, huwa na rangi nyeupe au mara nyingine usio na rangi kabisa. Lakini, baada ya kukauka mara nyingi huacha madoa (alama)kwenye nguo ya ndani, kama ukiwa umevaa nguo nyeupe utaweza kuona kiurahisi zaidi. Madoa hayo ni kitu cha kawaida kabida kisichohitaji kuwa na hofu ikiwa:

  • haina harufu yoyote
  • Hauambatani na kuwashwa au uke kuwaka moto

Ikiwa ute unaotoka una harufu mbaya au unahisi kuwashwa au uke kuwaka moto, au una wasiwasi yoyote kuhusu utokaje wake, basi ni muda muafaka kuwasiliana na daktari wa magonjwa ya wanawake aliye karibu nawe. Pia unaweza kuwashiliana na Daktari wa afyaclass kwa njia ya mitandao.

Muundo wa ute

Kwa maumbile ya mwanamke aliyepevuka, Ute ni majimaji ya kawaida kama vile mate.Lakini kabla hatujaendelea inabidi tujue, kwanini mwili wa mwanamke hutengeneza huu ute? Ute huu ni sehemu ya kawaida katika kulinda na kuhifadhi viungo vya uzazi vya mwanamke.Utando wa ute wa uke na tezi kwenye shingo ya kizazi hutoa majimaji ili kudumisha afya ya viungo vya uzazi.

Kwa kawaida, ute huu huundwa na vitu vifuatavyo, Ute wa njugumono (Mucus secretions) unatengenezwa na tezi za shingo ya kizazi na tezi za Bartholin, Maji maji yanayopita kupitia ukuta wa mishipa (vessel walls) yanayosambaza damu kwenye viungo vya uzazi, Ute unaotengenezwa na tezi za mafuta na tezi za jasho katika sehemu ya nje ya uke, Seluli zilizokufa kutoka kwenye epiteliamu ya uke na shingo ya kizazi, Makoloni makubwa ya bakteria, ikiwa ni pamoja na wale wa manufaa ambao huzuia maambukizi kuzaliana na kudumisha kiwango cha pH cha uke kuwa cha asidi.

Aina za ute

Baada ya kuangalia msingi wa ute na muundo wake, sasa tuangalie aina za ute na maana zake. Ikimbukwe kuwa, kiwango na na aina ya ute unaotoka hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Pia,rangi, muundo, na wingi pia unaweza kubadilika kutoka siku hadi siku, kulingana na hatua ya mzunguko wa hedhi ya mtu:

Siku 1-5: Mwanzoni mwa mzunguko, mara nyingi huwa na ute mwekundu au wa damu wakati mwili unaandaa utando wa damu kwenye mji wa kizazi (uterine lining).

Siku 6-14: Baada ya kipindi cha hedhi, mtu anaweza kugundua ukeni kuna utokaji wa ute kidogo kuliko kawaida. Kadiri yai linavyoanza kuendelea na kukomaa, ute wa shingo ya kizazi utakuwa wa rangi ya mawingu na mweupe . Unaweza kuonekana kuwa wa kunata.

Siku 14-25: Siku chache kabla ya uchavushwaji, ute utakuwa mwepesi na wenye kunata, kama sehemu nyeupe ya yai nyakati hizi kuambatana na ongezeko la hamu ya kufanya tendo la ndoa. Baada ya uchavushaji, ute utarejea kuwa wa rangi ya mawingu au  mweupe ,

Siku 25-28: Ute wa shingo ya kizazi utapungua na mtu atauona kidogo kabla ya kuanza kwa kipindi cha hedhi kingine.

 

Nyekundu

Hii mara nyingi huwa ni nyekundu iliyopooza au ile inayokaribia rangu ya kutu. Nyekundu mara nyingi ni husababishwa na damu inayotoka wakati wa hedhi. Kwa kawaida, wanawake hupata hadi kila baada ya siku 28, lakini ni jambo la kawaida kupata hedhi kati ya siku 21 hadi 35. Na wengi hukaa kwenye hedhi kwa muda wa siku 3 hadi 5. Endapo utaona damu katika kipindi siyo cha kawaida, basi unashauriwa kuwasiliana na daktari ingawa ni kitendo cha kawaida kwa wanawake wengi kutokwa na damu katikati ya kipindi cha hedhi (intermenstrual bleeding), kuna baadhi ya muda, inaweza kuwa ni ishara ya tatizo la kiafya.

Kwa mtu yoyote aliyefikia ukomo (monopause) na hajawahi kupata hedhi kwa kipindi cha mwaka mmoja au zaidi, halafu ikatokea akaona ute wa rangi nyekundu / damu ya hedhi, anashauriwa kuonana na daktari haraka kwani inaweza kuwa ni ishara ya ugonjwa wa saratani ya utando wa kizazi (endometrial cancer) 

 

Nyeupe

Ute huu huwa na rangi inayoanzia nyeupe, inaenza maziwa hadi njano. kama hauna dalili nyingine yoyote, basi ute mweupe ni inshara ya ute wa kawaida kama kilainishi shemu ya uzazi. Hata hivyo, ikiwa utoaji wa nyeupe una muundo kama wa jibini , maziwa au unakuja na harufu kali, inaweza kuashiria maambukizi hivyo unatakiwa anapaswa kumwona daktari.

Ute mweupe, mzito, wenye harufu kali mara nyingi unaashiria maambukizo ya fangasi (yeast infection), ambayo pia inaweza kusababisha kuwashwa au kuchomachoma.

 

Njano-Kijani

Ikiwa ute una rangi ya njano iliyofifia sana, inaweza isiwe ni ishara ya tatizo.  Hii inawezekana zaidi, haswa ikiwa rangi hiyo inahusiana na mabadiliko katika lishe au virutubisho vya chakula.

Ikiwa ute una rangi ya njano iliyokoza, au njano-kijani au kijani, inaashiria kuna maambukizi ya bakteria au magonjwa ya zinaa (STI). Tafadhali muone daktari mara moja ikiwa utoaji wa ukeni ni mzito au umegandaganda, au una harufu mbaya.

 

Pink:

Ute unaweza kuwa pinki iliyopooza au ile iliykoza,. Mara nyingi hii huwa imechanganyika na damu kidogo. Utoaji wa ute wenye rangi ya pinki mara nyingi hutokea kidogo kabla ya kipindi cha hedhi. Lakini, pia inaweza pia kuwa ni kiashiria cha awali cha uwepo wa ujauzito.

Baadhi ya watu wanaweza kutoa damu kidogo baada ya uchavushaji, ambayo pia inaweza kusababisha ute kuwa wa rangi ya pinki. Utoaji wa pinki unaweza kutokea baada ya kufanya tendo la ndoa ikiwa tendo lenyewe limeleta nyufa ndogo au vijijeraha katika uke au shingo ya kizazi.

Hauna Rangi

Ute wa kawaida huwa hauna rangi au mweupeoaji wa kawaida wa ukeni kwa kawaida ni wazi au mweupe. Unaweza kuwa na unyevu au muundo wa utakasa wa yai.

Kijivu

Utoaji wa ute wa rangi ya kijivu sio dalili nzuri kiafya na inaweza kuwa dalili ya maambukizo ya bakteria wanaoitwa bacterial vaginosis (BV).

Kawaida, maambukizi ya bakteria wa BV huambatana na dalili nyingine, ikiwa ni pamoja na:

  • Kuwashwa
  • Kuhisi kuchomwachomwa
  • Harufu kali
  • Kuvimba karibu na vulva au sehemu ya nje ya uke

Mtu yeyote mwenye ute wa kijivu anapaswa kumwona daktari mara moja. Baada ya kuthibitisha ugonjwa huo, kwa kawaida daktari humpa mgonjwa dawa za kuua bakteria (antibiotiki) kwa ajili ya matibabu ya BV. Epuka kutumia madawa ya antibiotiki bila kuandikiwa na daktari kwani kila dawa hutumia kulingana na ukubwa wa tatizo, aina ya ugonjwa na sababu nyingine zaidi za kitabibu ambazo huamuliwa na daktari baada ya kuona hali halisi ya ugonjwa na mgonjwa.

Mwanamke anaweza kuona ute msafi, unaoteleza sana siku chache kabla ya cuhavushaji (ovulation), wakati wa kujamiiana, na wakati wa ujauzito. 

Je ni kwa kiwango gani huwa ni kawaida?

Kwa mwanamke mwenye Afya njema, kwa kawaida hutoa wastani kati ya mililita 1 hadi 4 ya ute kila ndani ya masaa 24. Hata hivyo, kiasi hicho kinaweza kutofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu, kwa hvyo ikiwa utapata zaidi ya hapo inawezekana kabisa ni kawaida.

Pia, ni muhimu kukumbuka kwamba utoaji wa ute huongezeka sana wakati wa uchavushaji (kuwa na ute mwingi), ujauzito, na unapotumia vidonge vya uzazi wa mpango.

Ute wakati wa kujamiiana

Lengo kuu la ute kwenye sehemu za siri za mwanamke ni kufanya kuwe na unyevunyevu. Lakini ute huu wa kawaida hata pale unapokuwa umetoka katika kiwango chake cha juu kabisa (sanasana wakati wa uchavushaji), bado hauna uwezo wa kufanya sehemu za siri kuwa zimeloa vya kutosha kwa ajili ya kitendo cha kujamiiana. Hivyo kunahitajika ute mwingine wa ziada kuhakikisha kunakuwa na mtelezo wa kutosha.

Wakati wa tendo la ndoa, sehemu kubwa ya kiungo cha uzazi cha mwanamke kinakuwa kimepata damu ya kutosha hivyo hufanya vijimishipa vya shemu hii kutanuka kitendo kinachosababisha majimaji kupita kwa urahisi. Tezi za Bartholin zinazopatikana kwenye mashavu ya uke (ulvar vestibule) pia tezi za Skene zinazopatikana kwenye mrija wa mkojo (urethra) zote zinatumika kutengeneza ute ute.

Uteute huu husaidia kuongeza mtelezo wakati wa tendo la kujamiiana na kupunguza michubuko na msuguano wakati wa tendo.Kiwango halisi cha ute ute huu hutegemeana na mtu, umri, kiwango cha homoni and tarehe za hedhi. 

Wakati gani nimuone daktarin? 

Unatakiwa kuwahi kumuona daktari ikiwa utahisi ute una harufu au muonekano ambao sio wa kawaida.Pia anapaswa kutafuta huduma ya matibabu ikiwa unapata dalili kama vile:

  • Kuwashwa
  • Maumivu au kujisikia vibaya
  • Ute unaofanana na jibini cha krimu
  • Kutokwa damu kati ya hedhi au baada ya ukomo wa hedhi
  • Kutoka damu mara kwa mara baada ya tendo la ndoa
  • Ute wa rangi ya kijivu, kijani, au manjano
  • Harufu kali ukeni
  • Maumivi makali wakati wa kukojoa

Daktari atafanya uchunguzi wa viungo vya uzazi vya mwanamke (pelvic exam). Wanaweza pia kuhitaji kuchukua sampuli ya ukeni kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara.

Maswali ya Mara Kwa Mara: (FAQ)

Je, ni kawaida kwa wasichana wadogo kutokwa na ute?

Ndiyo, wasichana wa kila umri wanaweza kutokwa na ute, kawaida kwa kiasi kidogo hadi wanapokaribia kuingia kwenye umri wa kupevuka (Kuvunja ungo). Pia, huwa unatofautiana katika kiasi na rangi (kutoka hamna rangi hadi manjano au nyeupe). Hakuna haja ya wasiwasi isipokuwa ikiwa haueleweki, una rangi nyingine, au harufu isiyo ya kawaida.

Nawezaje kuzuia ute?

Utoaji wa ute ni jambo la kawaida na muhimu kwa afya ya uzazi wa kike. Hakikisha hamna harufu, au rangi zisizo za kawaida, pia ukiwa hauwashwi hauoni au kuchomwachomwa, hakuna haja ya kuchukua hatua yoyote.

Je, utokaji wa ute ni dalili ya ujauzito?

Ikiwa utokaji wa ute umeongezeka kwa kiasi na ni mwepesi, wa maziwa, na una harufu nyepesi, inaweza kuwa dalili ya ujauzito wa awali. Hii inaitwa leukorrhea na inaweza kujitokeza mapema kama wiki moja hadi mbili baada ya kushika ujauzito. Wakati wa ujauzito, utoaji wa ute utabadilika kulingana na muundo, kujirudia (frequency), na kiasi.

Umri gani Wasichana wanaanza kutokwa na ute?

Kwa kawaida wasichana huanza kupevuka kuanzia miaka 8 hadi 13. Lakini, baadhi ya vijana huanza kuonyesha dalili za ujana nje ya muda huo. Kwa ujumla, hedhi huanza takriban mwaka mmoja baada ya kuvunja ungo, ambayo mara nyingi hutokea akiwa bado mdogo sana.

Ni rangi gani ya ute inayohusiana na fibroids?

Fibroid ya kizazi (pia inaitwa leiomyoma, fibromyoma, au myoma) kwa kawaida ni ukuaji usio wa kansa ndani ya kizazi. Ute unaohusiana na fibroids unaweza kuwa kuanzia usio na rangi hadi mweupe au rangi ya damu hadi kijivu au kahawia. Kutokwa na damu nje ya kipindi cha hedhi ni jambo la kawaida kwa watu wenye fibroids.

Nini husababisha utokaji wa ute mwingi?

Utoaji wa ute zaidi ya kiwango cha kawaida inaweza kuwa ishara ya:

  • uchavushaji
  • Athari ya mzio
  • Msongo wa mawazo
  • Homoni kutokuwa kwa uwiano
  • Matumizi ya antibiotics
  • Matumizi ya dawa za kuzuia mimba

Je, ute mweupe ni ishara ya hedhi?

Ndiyo, ute mzito, mweupe, wa maziwa ni ishara ya kawaida ya kukaribia kipindi cha hedhi kinakaribia. Hiyo ni matokeo ya viwango vya juu vya progesterone, homoni inayosimamia ujauzito na mzunguko wa hedhi. Aina hii ya utokaji wa ute inaaminika kuwa ni ya kawaida ikiwa haiendani na harufu mbaya. Kwa kulinganisha, wakati viwango vya estrogeni vinaongezeka, ute huwa huwa hauna rangi na unavutika. via: Tanzmed

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!