Unaweza kufanya mapenzi na mtu mwenye ukimwi

Unaweza kufanya mapenzi na mtu mwenye ukimwi

Kuna njia nyingi ambazo hutumika ili kusaidia kuzuia maambukuzi ya Virusi vya ukimwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine wakati wa kufanya mapenzi,

Kama umepima wewe na mwenza wako,Moja wenu kapata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, hakikisheni mnapata Ushauri wa kutosha wa jinsi ya kuishi pamoja ili kuzuia maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Hivi ni Vitu vya msingi sana vya Kuzungatia ikiwa mpo kwenye hali kama hii;

1. Hakikisheni mpo kwenye tiba,

Moja ya njia rahisi na inayofanya kazi ni kuhakikisha mwenza wako yupo kwenye matibabu na anafuata kanuni zote za Tiba ya HIV.

hii inasaidia kupunguza maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine(An undetectable viral load makes HIV untransmittable).

2. Njia nyingine mpya ni kwa mwenza ambaye hana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutumia dawa zinazoitwa PrEP

Kwa mwenza ambaye yupo NEGATIVE Anaweza kutumia PrEP, Hizi ni dawa za kunywa(vidonge) ambavyo husaidia kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi kabla ya mtu kuwa kwenye mazingira ya hatari.

Na kwa mujibu wa tafiti mbali mbali PrEP zina uwezo mkubwa wa kufanya hivo.

3. Matumizi Sahihi ya kinga kama kondomu

Matumizi sahihi ya condomu kwa Mwanaume au mwanamke huweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kusambaza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

4. Jikinge na magonjwa mengine ya Zinaa(STI’s),

Ikiwa mwenza wako ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi(VVU), kuna uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa mengine ikiwemo ya Zinaa, kwa sababu ya kinga yake ya Mwili kuwa dhaifu Zaidi.

Hii huongeza hatari ya wewe kupata magonjwa mengine zaidi.

5. Mambi haya pia huweza kukuweka kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi;

  • Viral Load kuwa juu
  • Muda wa kufanya mapenzi
  • Kufanya mapenzi katika mazingira magumu(roughness of sex), hapa hakuna maandalizi ya kutosha, mnafanya kwa nguvu kama kukomoana, kuchubuana n.k

Moja ya vitu muhimu vya kuchunguza kwa mwenza wako ikiwa ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi(VVU) ni pamoja na VIRAL LOAD,

Kwa mujibu wa Utafiti mmoja ulionyesha kwa Watu ambao VIRAL LOAD ilikuwa chini uwezekano wa kusambaza maambukizi ulikuwa mdogo sana au sawa na Zero.

Utafiti huo Unasema;

 “The PARTNER study reported zero HIV transmissions after 900 couples had sex more than 58,000 times WITHOUT condoms. In this study undetectable viral load was defined as being less than 200 copies/m”.

Utafiti huu unaendelea kwa kusema; Hatari ya kupenya Virusi kwa Mtu anayefanya mapenzi bila kondomu na mtu ambaye ana kiwango cha juu cha virusi(HIGH VIRAL LOAD) inaweza kuwa juu Zaidi kama 1 kati ya 10 (hatari 10%). Lakini hatari ni sifuri kwa mtu ambaye anatumia matibabu(dawa) na ambaye ana kiwango cha chini sana cha virusi(LOW VIRAL LOAD) au kisichoonekana.

Mambo ya kuzingati wewe na Mwenza wako ikiwa mmoja wenu ana Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi

Je, wewe na mwenzi wako mnaweza kuchukua tahadhari gani?

Kuna tahadhari kadhaa ambazo wewe na mwenzi wako mnaweza kuchukua ili kuzuia kuambukizwa au kusambaza VVU kupitia ngono.

(1) Hakikisheni mnatumia njia za kujikinga kama condoms pamoja na njia nyingine

Mbinu za kujikinga kama vile kondomu huweza kusaidia kuzuia michubuko na kugusa maji maji ya mwili wakati wa kujamiiana na mtu anayeishi na VVU.

Vikitumiwa  ipasavyo, vizuizi hivi vinaweza kuzuia uambukizaji wa VVU na magonjwa mengine ya Zinaa.

Kutumia vilainishi au mafuta ya kutosha kunaweza pia kusaidia kupunguza hatari ya VVU, pia – bila kusahau, kufanya ngono kuwa bora zaidi.

(2) Hakikisheni mnatumia dawa muhimu ikiwemo ART, PrEP, na PEP

Kuna dawa chache zinazoweza kusaidia kuzuia maambukizi ya VVU:

ART: Mtu anayeishi na VVU anaweza kutumia dawa zinazojulikana kama ART ili kumsaidia kuwa na afya bora na kuzuia uambukizaji wa VVU.

Watu wengi wanaotumia dawa kama ilivyoagizwa wanaweza kupunguza kiwango chao cha virusi hadi kiwango kisichoonekana.

PrEP: Hii ina maana ya pre-exposure prophylaxis, PrEP ni dawa ambayo mtu asiye na VVU anaweza kutumia kabla ya kuingia kwenye mazingira hatarishi ili kupunguza hatari ya kuambukizwa VVU kwa asilimia 99.

PEP: Hii ina maana ya Post-exposure Prophylaxis, PEP hutumika baada ya kuwa kwenye mazingira hatarishi ya kuambukizwa,

au PEP, ni regimen ya dawa inayoweza kusaidia kupunguza hatari ya kuambukizwa VVU baada ya kuwa kwenye mazingira hatarishi ya kuweza kuambukizwa inapoanzishwa au kutumika ndani ya saa 72.

(3) Jengeni Utaratibu wa kufanya Vipimo mara kwa mara ikiwemo Vipimo vya magonjwa ya Zinaa(STIs)

Ni muhimu kwako na kwa mwenzi wako kupima magonjwa ya Zinaa mara kwa mara. Utambuzi wa mapema na matibabu ya magonjwa ya zinaa inaweza kupunguza hatari ya matatizo.

Kuwa na magonjwa ya zinaa kunaweza kuongeza hatari ya kuambukizwa VVU.

(4) Fahamu Dalili kubwa za Ukimwi na magonjwa mengine ya Zinaa(STIs)

Kufahamu kuhusu dalili za magonjwa ya Zinaa(STI) ni muhimu kwa mtu yeyote anayeshiriki ngono.

Muone mtaalamu wa afya ukigundua mojawapo ya haya:

  • kutokwa na uchafu usio wa kawaida kutoka kwa njia ya haja kubwa, uume au uke
  • kutokwa na damu kusiko kwa kawaida ukeni, kama vile kutokwa na damu baada ya kujamiiana au katikati ya mzunguko wa hedhi
  • Kuhisi kuungua au maumivu wakati wa kukojoa
  • Kuhisi kukojoa mara kwa mara
  • Kuwa na vidonda au malengelenge kwenye au karibu na sehemu zako za siri,eneo la haja kubwa(mkundu) n.k
  • Kuwa na upele kwenye au karibu na sehemu zako za siri au mkundu
  • kuwashwa sehemu za siri n.k

(5) Hakikisheni mnapata Ushauri wa kutosha wa jinsi ya kuishi pamoja kutoka kwa wataalam wa afya.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!