Ticker

6/recent/ticker-posts

Utafiti: Kila mwanamke 1 kati ya 3 hupatwa na tatizo la kiafya wakati wa kujifungua.



Zaidi ya mwanamke 1 kati ya 3 duniani mara nyingi hukutwa na matatizo ya kiafya pindi wanapojifungua hii inaweza kutokea ndani ya mwezi kulingana na utafiti uliofanywa na (Lancet Global Health).

Matatizo hayo yanayowakumba wanawake hutokea nyakati mbalimbali ikiwemo:

  • wakati wa kujamiana ni 35%

maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo 32%

  • Kushindwa kujizuia mkojo 8%-31%
  • Kushindwa kujizuia choo 19%
  • Woga wakati wa kujifungua 6%-15%
  • Maumivu ya sehemu inayounganisha eneo la haja kubwa na ndogo(perineal pain) 11%
  • Msongo wa mawazo 11%-17%
  • Wasiwasi 9%-24%
  • Kushindwa kupata ujauzito mwingine baada ya kujifungua 11%

Matatizo mengine yanayowakumba wanawake wakati wa kujifungua ni pamoja na;

  1. Matatizo yanayotokea kwenye via vya uzazi mfano pelvic organ prolapse.
  2. Mwanamke kupata msongo wa mawazo kutokana na maumivu aliyopata baada ya kujifungua(
    posttraumatic stress disorder).
  3. Tatizo la tezi ya shingoni kutokufanya kazi vizuri(thyroid dysfunction).
  4. Tatizo la tishu za matiti kuvimba kutokana na maambukizi ya bakteria n.k hali inayosababisha maumivu na kuvimba kwa matiti hasa wakati wa kunyonyesha(mastitis).
  5. Tatizo la kuumia kwa neva.
  6. Tatizo la mama kupata hali ya ukichaa baada ya kujifungua(psychosis).

Uchunguzi unasema: wanawake wengi humuona daktari wiki ya 6 mpaka 12 baada ya kujifungua na kwa nadra sana baadhi yao ndio huweza kumuelezea daktari juu ya matatizo yanayowapata baada ya kujifungua, kwa baadhi ya matatizo hudhihirika na kuonekana zaidi kuanzia wiki ya sita na kuendelea.

 

 



Post a Comment

0 Comments