Wanafunzi Sudan kuhamishiwa hospitali ya Temeke

Wanafunzi Sudan kuhamishiwa hospitali ya Temeke

WANAFUNZI 20 wa udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Tiba, Sayansi na Teknolojia (UMST) cha Khartoum nchini sudan wanatarajia kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke(TRRH) kama moja ya hatua ya kuongeza ujuzi katika fani ya udaktari baada ya kukamilisha kipindi chao cha mafunzo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

Uhamisho huo unatarajia kufanyika kuanzia  tarehe 02 Januari 2024 kwa kuzingatia lengo la kuwawezesha kupanua ujuzi wao na kujifunza mazingira tofauti ya utunzaji wa afya.

Aidha,Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, Dk Joseph Kimaro,amesema,

Wanafuraha kubwa kuwakaribisha wanafunzi hao  na wapo tayari kutoa ushirikiano na kuhakikisha wanafunzi hao wanapata elimu bora na mafunzo

“Tunafurahi kuwakaribisha wanafunzi hawa wa UMST katika timu yetu ya wataalamu wa afya kwani tupo tayari kutoa ushirikiano kwa wanafunzi na kuhakikisha wanapata elimu bora na mafunzo sahihi yatakayowawezesha kuwa madaktari wenye ujuzi” ameyasema hayo mara baada ya mazungumzo makini kati uongozi wa TRRH, na Profesa Mamoun Homeida kutoka Chuo cha Tiba, Sayansi na Teknolojia (UMST).amesema Joseph kimaro

Wanafunzi hawa wana matarajio ya kujiunga na idara mbalimbali za hospitali hiyo, kama vile idara ya mifupa, watoto, upasuaji, upasuaji njia ya mkojo, magonjwa ya ndani, na idara ya wanawake na uzazi. Kila idara inawakilisha fursa kwa wanafunzi hawa kuendeleza stadi zao na kujenga misingi imara ya ujuzi wa udaktari.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!