‘Nyumba ilikuwa na fujo sana’
Kunywa chai na sokwe na kutoka na mnyama mwingine kwa ajili matembezi ilikuwa sehemu ya maisha ya kila siku kwa familia ya Graham Clews.
Familia yake ilikuwa na wanyama wengi kiasi kwamba walifungua bustani ya wanyama nyumbani kwao Warwickhire, Uingereza, mwaka wa 1966.
Wanyama wadogo na nyani walilelewa ndani ya nyumba na watoto wa Graham walikua pamoja na watoto wa sokwe.
Ni Karibu miaka 40 sasa baada ya bustani yao ya wanyama kufungwa, sasa familia hiyo imebaki na masanduku ya picha na sehemu za magazeti yenye picha.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!