Ticker

6/recent/ticker-posts

WHO:Hatari kubwa ya Magonjwa ya mlipuko Kusambaa Gaza



WHO:Hatari kubwa ya Magonjwa ya mlipuko Kusambaa Gaza.

Shirika la Afya Duniani WHO linaangaza athari mbaya za mzozo unaoendelea likisema kuna hatari kubwa ya magonjwa ya milipuko kusambaa.

Tangu Oktoba 7, 2023 mapigano yalipoanza, kumekuweko na wagonjwa 179,000 wa magonjwa ya njia ya hewa, wagonjwa 136,000 wa kuhara miongoni mwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, na wagonjwa 55,400 wa vidonda na chawa.

Tangu shambulio la Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba 2023, lililosababisha vifo vya watu 1,200 na wengine 240 watekwe nyara, mapigano kwenye ukanda wa Gaza, na mashambulizi kutoka angan ina ardhini  na vile vile baharini yanayofanywa na jeshi la Israel (IDF) yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 22,000 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto, kwa mujibu wa maafisa wa afya wa Palestina.

Takwimu za IDF zilizotolewa Desemba 30, 2023 zinadokeza kuwa askari 168 wa Israel wameuawa tangu kuanza kwa operesheni za kijeshi za ardhini huko Gaza na wengine 955 wamejeruhiwa.

Wizara ya afya Gaza nayo inaripoti kuwa zaidi ya wapalestina 200 wameripotiwa kuuawa tangu jana jumatatu pekee hadi leo, huku wengine 338 wamejeruhiwa.

Maelfu wahofiwa kufa

Wakati huo huo, WHO katika taarifa yake mpya inasema watu wengine 7,000 kwa sasa hawajulkani waliko au wamefukiwa kwenye vifusi.

Ripoti hiyo pia inasema watu 600 wameuawa kufuatia mashambulizi 300 kwenye hospitali tangu Oktoba 7, mashambulizi ambayo yameharibu hospitali 26 na magari ya wagonjwa 38.

Kati ya watu milioni 1.93 waliofurushwa makwao Gaza, 52,000 ni wajawazito ambao wanajifungua watoto 180 kila siku, kwa mujibu wa WHO. Imeelezwa pia wagonjwa 1,100 wanahitaji huduma ya kusafisha figo kila siku, 71,000 ni wagonjwa wa kisukari na 225,000 wanahitaji tiba dhidi ya shinikizo la damu.



Post a Comment

0 Comments