#BREAKING: Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa (70) amefariki Dunia leo
#BREAKING: Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa (70) amefariki Dunia leo.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa (70) amefariki Dunia leo February 10,2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais , Dkt. Philip Mpango ametangaza taarifa za kifo cha Lowassa muda huu akiwa LIVE kupitia TBC.
Lowassa alihudumu katika nafasi ya waziri mkuu kati ya mwaka 2005 hadi 2008 chini ya uongozi wa rais wa zamani Jakaya Kikwete.
Mwaka wa 2015 aliwania urais kwenye uchaguzi mkuu akiwa mgombea wa chama cha (CHADEMA) ambapo alishindwa na aliyekuwa rais hayati John Magufuli.
Serikali imetangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa kuanzia leo Jumamosi.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!