Katika wiki nne tu za kwanza za mwaka, nchi 10 za Afrika ziliripoti visa zaidi ya 26,000 na vifo 700 kutokana na KIPINDUPINDU

Katika wiki nne tu za kwanza za mwaka, nchi 10 za Afrika ziliripoti visa zaidi ya 26,000 na vifo 700 kutokana na KIPINDUPINDU.

Katika wiki nne tu za kwanza za mwaka, nchi 10 za Afrika ziliripoti visa zaidi ya 26,000 na vifo 700, ambavyo ni karibu mara mbili ya idadi iliyoripotiwa mwaka jana kwa kipindi kama hicho.

Zambia na Zimbabwe ndizo zilizoathiriwa zaidi, lakini Msumbiji, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ethiopia na Nigeria pia zinakabiliwa na “milipuko ya kasi”, na hatari kubwa ya kusambaa zaidi, Dk. Braka alisema.

Je,Ugonjwa wa kipindupindu unaweza kuzuilika na kutibiwa?

“Tutaendelea kuona rekodi zikivunjwa ikiwa watu hawana maji safi na vifaa vya usafi,”,” alielezea. “Kipindupindu kinaweza kuzuilika na kutibika. Hakuna mtu, tena, anayepaswa kufa kutokana nayo.”

Kuongezeka kwa mafuriko yanayohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa kumeongeza kuenea kwa kipindupindu, ugonjwa unaoweza kuzuilika. Vimbunga na ukame zaidi pia vimepunguza upatikanaji wa maji safi, na hivyo kutengeneza mazingira bora ya kipindupindu kustawi.

Licha ya uhaba wa chanjo za kipindupindu duniani kote, WHO inaunga mkono juhudi za chanjo nchini Zambia, ambapo zaidi ya watu milioni 1.7 wamechanjwa. Kampeni pia inaendelea nchini Zimbabwe, ambayo inatarajia kutoa ulinzi kwa watu milioni 2.3.

WHO pia imetuma zaidi ya wataalam 100 wa matibabu na kupeleka vifaa vya dharura katika maeneo yaliyoathirika nchini Zambia na Zimbabwe.

Zaidi ya tani 30 za vifaa vya dharura tayari vimewasilishwa kwa nchi zote mbili, ikiwa ni pamoja na vifaa vya kipindupindu pamoja na rehydration salts, huku msaada zaidi ukiendelea.

Source:UN

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!