Maadhimisho ya siku ya Saratani ya Watoto Duniani

Idara ya saratani Bugando imeadhimisha siku ya saratani za watoto duniani leo Februari 15,2024 kwa kutoa elimu kwa wazazi wa watoto wenye Saratani, maadhimisho haya yameambatana na kauli “ Kuongeza ufahamu wa saratani za watoto”.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkurugenzi wa Desk and Chair foundation
Bw.  Sibtain Maghjee ambae ni Mgeni rasmi amesema takwimu zimeonesha  ukubwa wa tatizo hili katika jamii yetu “Watoto 400,000 chini ya miaka 18 Duniani wanagundilika na Saratani kila mwaka” ili kukabiliana na tatizo hili serikali yetu kupitia Wizara ya Afya imeendelea kujenga miundombinu, Kufundisha wataalamu na kutoa vifaa tiba ili kusaidia wagonjwa wa saratani, pia amelipongeza Baraza la Maaskofu ( TEC),Wadau mbalimbali kwa uwezeshaji mkubwa uliofanikisha uanzishwaji na uboreshwaji wa huduma za matibabu ya Saratani kwa watanzania wote na hasa kwa watoto wetu, pamoja na hayo amesema elimu imeendelea kutolewa kwa jamii ili kujiepusha na vichocheo vya saratani, Ufahamu wa kugundua dalili za awali za saratani na kwenda kuchunguzwa mapema. Aidha ameiomba hospitali kuanzisha radio ambayo itasambaza elimu za afya kwa jamii kwa haraka ili wananchi waweze kupata uelewa juu ya magonjwa mbalimbali kwani radio inasaidia kufikisha ujumbe kwa haraka zaidi.

Nae Mkurugenzi wa huduma saidizi Dkt. Cosmas Mbulwa  amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali Dkt Fabian A. Massaga ameishukuru na kuipongeza serikali kwa kushirikiana na hospitali katika kuhakikisha watoto wanapata matibabu stahiki pia amewapongeza Idara ya Saratani ambao wanafanya kazi kwa juhudi kubwa ili kuhakikisha watoto hawa wanafikia ndoto zao kwa kupata matibabu stahiki na kusema Hospitali inaendelea kutoa elimu juu ya magonjwa ya saratani hasa maeneo ya vijijini.

Sambamba na hayo Daktari Bingwa Bobezi wa Magonjwa ya saratani za watoto Dkt. Heronima Joas amesema “Siku ya Saratani za watoto hutukumbusha ujasiri na uthubutu wa watoto katika kupambana na changamoto za Saratani mbalimbali. ” Akihamasisha wananchi waliohudhuria katika maadhimisho haya kuwamabalozi kwa Wengine kwa elimu waliyoipata.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!