Bi. Nuru Mshana mkazi wa Ilala Dar es salaam ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kumtolea mtoto wake kipande cha plastiki ambacho kilikuwa kinamsumbua muda mrefu na kusababisha kukohoa na kupata changamoto ya kupumua usiku.
Bi. Nuru amesema mtoto wake mwenye umri wa miaka 7 alimeza kipande cha plastiki wakati akiwa anacheza na kumsababishia kupata madhara kwenye mfumo wa upumuaji.
“Mtoto wangu alipomeza kipande cha plastiki tulijaribu kumtoa hatukufanikiwa, mara baada ya muda alianza kukohoa tukampeleka tena hospitali madaktari walitueleza kwamba mtoto atakuwa na ugonjwa wa pumu hivyo alipatiwa dawa za pumu bila mafanikio yoyote” amesema Bi. Nuru
“Tuliona taarifa kupitia mtando wa kijamii ikionesha baadhi ya watu waliokuwa na changamoto ya kukohoa na walipofanyiwa uchunguzi walibainika kuwa walimeza vitu visivyokuwa vya kawaida ,hivyo na sisi tuliamua kumleta mtoto wetu hapa Muhimbili na alipofanyiwa uchunguzi madaktari waligundua kuwa alimeza kipande cha plastiki ”
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Mapafu na Mfumo wa Upumuaji Dkt. Jude Tarimo ambaye ameshiriki katika zoezi hilo ametoa wito kwa jamii kuwa makini na vitu wanavyoweka mdomoni kwakuwa plastiki ikiingia kwenye mapafu inaweza kusababisha kupata madhara mbalimbali hasa kwenye mfumo wa upumuaji.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!