Mwanafunzi amepata alama sawa na mwanafizikia Albert Einstein

“Sikutarajia kwamba ningepata alama za juu namna hiyo. Sikuamini. Mtihani ulikuwa rahisi sana, lakini kulikuwa na maswali kadhaa magumu.”

Mwanafunzi wa shule ya Sheffield amepata alama za juu katika mtihani wa kupima akili, amepata alama sawa na mwanafizikia na mwanasayansi nguli Albert Einstein.

Cyrus, mwenye umri wa miaka 12, alikosea maswali mawili tu ili kufikia alama ya Mensa ya 160, na sasa amekubaliwa katika jumuiya maarufu duniani ya IQ ya juu.

Alama hiyo inamweka sawa na Einstein na Stephen Hawking.

Cyrus, ambaye anataka kuwa mwanahisabati au mwanasayansi wa data, alisema “anajivunia” kwa alama hizi

Je wewe ulipata alama ngapi katika soma la hisabati.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!