Mwanasiasa kijana, umri miaka 29, auawa mchana kweupe alipokuwa akirekodi video kuhusu barabara
Mwanasiasa kijana, umri miaka 29, auawa mchana kweupe alipokuwa akirekodi video kuhusu barabara.
Diwani wa Equador aliuawa mchana kweupe mbele ya umati wa watu muda mfupi tu baada ya kumaliza mkutano.
Diana Carnero, mwenye umri wa miaka 29, alikuwa akiongoza mkutano wa baraza katika mji wa Naranjal huko Guayas Jumatano alasiri, Februari 7, na kurekodi video kuhusu hali mbaya ya barabara ndipo aliposhambuliwa.
Washukiwa wawili wa kiume walimwendea wakiwa kwenye pikipiki na kumpiga risasi kichwani kabla ya kukimbia, polisi walisema.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Ecuador ilisema itaongoza uchunguzi lakini hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa.
Ecuador iko katika mtego wa wimbi la uhalifu linalohusishwa na magenge ya ulanguzi wa dawa za kulevya.
Mwaka jana tu, mgombea urais aliuawa Ecuador. Wanasiasa wengine wa Ecuador pia wamenyongwa hivi majuzi.
Wiki mbili zilizopita Rais Daniel Noboa alitangaza hali ya dharura na vita halisi dhidi ya magenge hayo kwa kuidhinisha jeshi kuchukua hatua dhidi yao. Watu wengi wanakaa nyumbani,Shule na maduka yamefungwa huku askari wakizunguka katika mitaa ya miji mikubwa ya Ecuador.
Carnero aligombea chini ya Citizen Revolution Movement, chama cha siasa cha kisoshalisti cha kidemokrasia ambacho kiliundwa na wafuasi wa Rais wa zamani Rafael Correa na kuchaguliwa kuwa baraza la jiji la Naranjal mnamo Februari 2023.
Correa, ambaye alihudumu kama rais kutoka 2007 hadi 2017, alitoa pongezi kwa Carnero. kwenye X, mtandao wa kijamii ambao hapo awali ulijulikana kama Twitter.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!