Mwanaume wa Marekani anakaribia kutangazwa kuwa ameponywa VVU na saratani ya damu
Mwanaume wa Marekani anakaribia kutangazwa kuwa ameponywa VVU na saratani ya damu.
Paul Edmonds, mwenye umri wa miaka 68, kutoka California ambaye alitrend kwenye vichwa vya habari vya kimataifa mnamo 2023 alipotoa hadithi yake, bado hana athari za hali zote mbili miaka mitano baada ya kupandikizwa seli ambazo ziliondoa magonjwa yote mawili mwilini.
Katika makala mpya ya timu ya madaktari waliomtibu, madaktari walisema alipona rasmi saratani na miaka miwili kabla ya kutangazwa kuwa amepona VVU.
Safari ya matibabu ya Edmonds ilianza alipogundulika kuwa na UKIMWI mwaka 1988, wakati ambapo virusi hivyo viliua wanaume wengi wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.
Licha ya kuwatazama marafiki zake wengi wakifa kutokana na maambukizo hayo, hakufa, na aliishi hadi utambuzi mbaya wa leukemia mnamo 2018 nusura ukatize matumaini yake ya kuishi maisha marefu.
Alitibiwa saratani hiyo kwa tiba ya seli shina, ambayo inahusisha kuchukua nafasi ya seli zilizoharibiwa na chemotherapy na zile zenye afya kutoka kwa wafadhili, wakati madaktari waliona fursa ya kipekee: kupata wafadhili na mabadiliko ya jeni yanayokinzana na VVU.
Madaktari walitaka kujua kama wanaweza kuiga mafanikio ya wagonjwa wa awali ambao walikuwa wameripotiwa kuponywa VVU na saratani kwa njia hii.
Kulingana na kliniki ya City of Hope huko California, Edmonds ni mmoja wa watano walioshinda magonjwa yote mawili na mtu mzee zaidi kufanya hivyo.
‘Ninashukuru sana… siwezi kuwashukuru vya kutosha,’ Bw Edmonds alisema kuhusu madaktari wake katika kliniki ya City of Hope huko California.
Kupandikiza seli shina ni sehemu ya mwisho ya matibabu ya saratani ya damu kama vile leukemia na lymphoma.
Inatolewa wakati seli za shina zinazounda damu kwenye uboho wa mgonjwa zimeuawa na mionzi au chemotherapy.
Mnamo Novemba 2018, Bw Edmonds alianza matibabu,Alihitaji raundi tatu ili kufikia hatua nzuri, ambapo katikati ya Januari 2019 alifanikiwa.
Mwezi uliofuata alipokea seli kutoka kwa wafadhili wake.
Seli shina alizopewa zilikuwa na nakala mbili za mabadiliko ya nadra ya kijeni inayoitwa CCR5 delta-3, ambayo huwafanya watu kuwa sugu kwa VVU. Asilimia moja hadi mbili tu ya watu wana mabadiliko haya.
VVU hutumia kipokezi CCR5 kuingia na kushambulia mfumo wa kinga, lakini mabadiliko ya CCR5 huzuia virusi kuingia kwa njia hii.
Inakadiriwa kuwa watu milioni 36.3 wamekufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na UKIMWI tangu kuanza kwa janga hilo mnamo 1981.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!