Mwanzilishi benki ya Access afariki dunia.
Mwanzilishi wa Benki ya Access duniani, Herbert Wigwe (57) amefariki dunia kwa ajali ya helikopta iliyotokea California, nchini Marekani.
Benki ya Access yenye makao makuu nchini Nigeria ina matawi katika nchi za Tanzania, Congo, Ghana, Kenya, Uganda, Nigeria, Rwanda, Gambia, Guinea, Cameroon, Sierra Leone, Msumbiji, Botswana, Afrika Kusini, Zambia, Ufaransa na Uingereza.
Katika ajali hiyo iliyotokea juzi, Februari 10, 2024 saa nne usiku, pia imesababisha kifo cha mkewe, mtoto wake wa kiume na watu wengine watatu waliokuwa ndani ya helikopta ‘chopa’ hiyo.
Wigwe, mzaliwa wa Ibadan nchini Nigeria alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa Access Holding, ambayo ni kampuni mama ya Benki ya Access.
Herbert Wigwe akiwa na mkewe enzi za uhai wao
Chopa ya Wigwe ambaye pia ni mmiliki na mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Wigwe, ilikuwa ikielekea Las Vegas kabla ya kupata ajali mpakani mwa Nevada na California usiku wa Ijumaa.
Mamlaka ya anga nchini Marekani, imethibitisha hakuna aliyenusurika katika ajali hiyo na wanaendelea kuchunguza chanzo chake.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Afrika Magharibi, Rais wa Nigeria, Bola Tinubu ameeleza kusikitishwa na ajali hiyo akisema kifo cha Wigwe ni pigo kwa sekta ya benki nchini Nigeria na Afrika kwa ujumla.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!