Mzee Mwinyi alazwa hospitali akiugua maradhi ya Kifua

Mzee Mwinyi alazwa hospitali akiugua maradhi ya Kifua.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi amelazwa hospitali akiugua maradhi ya kifua na anaendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Msemaji wa familia Abdullah Ali Mwinyi imeeleza kuwa,
kutokana na ushauri wa madaktari, familia imeona ni vema apate faragha akiwa anapatiwa matibabu.

“Hivyo familia inaiomba jamii kumkumbuka kwenye Dua, Sala, na Maombi.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie shifaa ya haraka Mzee wetu pamoja na wagonjwa wengine wote wanaokabiliwa na maradhi mbali mbali”. Imesema taarifa hiyo ya
Msemaji wa familia ya Mzee Mwinyi.

Via:@tbc_online

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!