Rais wa Namibia Hage Geingob amefariki dunia leo

Rais wa Namibia Hage Geingob amefariki dunia leo Feb 04,2024 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Lady Pohamba iliyopo Mji Mkuu wa Nchi hiyo Windhoek.

Ofisi ya Rais wa Namibia imethibitisha taarifa hiyo na kusema amefariki wakati Mkewe Monica Geingos na Mwanae wakiwa karibu nae.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 82 aligunduliwa kuwa anaugua saratani na alitangaza hali yake mbele ya umma mwezi uliopita na baadaye ofisi yake ilitangaza kwamba atasafiri kuelekea Marekani kupata matibabu, itakumbukwa pia alifanyiwa upasuaji wa moyo mwaka jana, na mwaka 2014 alitangaza kuwa amepona saratani ya tezi dume.

Geingob aliapishwa kuwa Rais mwaka 2015 na alikuwa anatumikia awamu yake ya pili na ya mwisho ya uongozi.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!