TUKIO: Mwanamke atoroka na mtoto wa mwajiri wake kisha kumuuza

TUKIO: Mwanamke atoroka na mtoto wa mwajiri wake kisha kumuuza.

Mwanamke mmoja nchini Nigeria aliyetoroka na mtoto wa mwajiri wake akiri kumuuza mtoto huyo kwa N800k,

Mjakazi huyo ambaye hivi majuzi aliajiriwa na familia kupitia wakala amemuuza mtoto ambaye alikuwa ameajiriwa kumlea.

Mjakazi huyo, aliyetambulika kama Ruth Okezie, aliripotiwa kutoroka na mtoto huyo kutoka kwenye nyumba ya Shomolu mwendo wa saa mbili asubuhi. Jumamosi asubuhi, Februari 3.

Baada ya taarifa ya mtu aliyepotea kutangazwa kwenye mitandao ya kijamii, kijakazi huyo alipatikana Ikorodu, bila mtoto huyo,

Kwa sasa amekiri kumuuza mtoto huyo kwa shilingi N800,000.

Mtumiaji mmoja wa mtandao wa X(twitter) aliye karibu na hali hiyo, ambaye alishiriki hadithi hiyo, alisema mtoto bado hajapatikana.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!