Ufaransa imerekodi zaidi ya vifo 5000 vilivyotokana na joto mwaka wa 2023

Ufaransa imerekodi zaidi ya vifo 5000 vilivyotokana na joto mwaka wa 2023 

Zaidi ya watu 5,000 walikufa nchini Ufaransa kutokana na joto la kiangazi mwaka jana, mamlaka ya afya ilisema Alhamisi, Februari 8.

“Kila mtu ameathirika,” Caroline Semaille, mkuu wa wakala wa afya ya umma wa Ufaransa, aliwaambia waandishi wa habari alipokuwa akiwasilisha ripoti juu ya vifo vinavyotokana na joto mwaka jana.

Majira ya joto ya mwaka 2023, yaliwekwa alama na kulikuwa na mawimbi manne ya joto ikiwa ni pamoja na kipindi cha mwezi Agosti na Septemba, majira haya ya joto yalikuwa ya nne kwa joto zaidi kwenye rekodi nchini Ufaransa.

Pia sio nchini Ufaransa pekee,Mwaka wa 2023 ulikuwa mwaka wa joto zaidi kuwahi kurekodiwa ulimwenguni.

Kulingana na shirika la afya ya umma la Ufaransa, vifo 5,167 au vifo vitatu kati ya kila vifo 100 vilitokana na joto msimu uliopita wa joto. Kati ya vifo hivyo, karibu watu 3,700 walikuwa na umri wa zaidi ya 75.

Joto kali limekuwa likisumbua mifumo ya huduma za afya, likiwakumba wazee, watoto wachanga na watoto wakubwa.

Kwa kulinganisha, karibu vifo 7,000 vilitokana na joto mnamo 2022, ingawa janga la coronavirus linaweza kuwa sababu pia.

Nchi hiyo imeweka miongozo madhubuti ya kukabiliana na wimbi la joto baada ya takriban watu 15,000 kufa wakati wa kiangazi cha 2003.

Ufaransa itakuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki mjini Paris kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11, na wataalam wanasema majira ya joto kali yanaweza kuleta matatizo kwa waandaaji.

Wanasayansi wameonya kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yanaleta tishio kwa maisha duniani, yakiashiria hali mbaya ya hewa ambayo inapiga zaidi kuliko hapo awali.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!