Wafanyakazi wa hospitali watuhumiwa kwa kukataa kumlaza mtoto mchanga kisa mama yake kavaa Hijabu

Wafanyakazi wa hospitali watuhumiwa kwa kukataa kumlaza mtoto mchanga baada ya mama yake kukataa kutoa Hijabu na kuvaa nguo maalum za kuingilia eneo hilo.

Vyombo vya habari vya Kiislamu vilizua hisia tofauti baada ya kuwashutumu wafanyikazi katika Hospitali ya Chuo Kikuu(UCH) Ibadan nchini Nigeria kwa kumkataa mtoto mchanga aliyezaliwa mgonjwa kutokana na kukataa kwa mama yake kutoa Hijabu yake.

Muslim News Nigeria ilishiriki video ya tukio hilo hospitalini.

Katika video hiyo, matabibu hao ambao walikuwa wamevaa nguo maalum(Scrubs), wanaonekana wakiwaeleza wazazi wa mtoto mchanga kuwa hakuna mtu anayeweza kuingia katika chumba cha wagonjwa mahututi (NICU) bila kubadilisha kuwa kama wao. Hii ni kuzuia kuenea kwa maambukizi kwa watoto wachanga.

Wahudumu wa hospitali hiyo pia walionyesha kuwa wao pia walikuwa wamevaa scrubs na kueleza kuwa ni sheria ya kuzuia kuenea kwa maambukizi na kuwalinda watoto wachanga ambao bado kinga zao ni hafifu sana.

Hata hivyo, baba wa mtoto huyo alikataa kusikiliza maelezo yao na kuwaambia wafanyakazi kwamba walipaswa kumweleza sheria kabla hajafanya malipo.

Video hiyo ilipokea maoni tofauti baada ya kuwekwa mtandaoni.

Mtumiaji mmoja wa mtandao wa X aliandika: “Wallahi, nitageuza mahali hapo juu chini. Hicho ni kituo cha serikali si cha kibinafsi.”

Hata hivyo, watumiaji wengi waliambia Muslim Media kwamba usalama wa watoto wengine hauwezi kuhatarishwa na mama mmoja.

Madaktari walipima uzito. Walieleza kuwa nguo ndefu kama vile Hijabu na nguo zinazovaliwa kutoka nje haziruhusiwi kuingia NICU.

Daktari mmoja aliandika hivi:

“Wakati nafanya kazi ICU kama intern, sikuingia ICU na nguo zangu za kazi, kulikuwa na scrubs na viatu vilivyowekwa kwa kila mtu nje, tukabadilisha.

“Tulifunika nywele zetu na kuvaa vinyago vya uso(masks)!!!!

“Hawa ni watoto wenye kinga ya chini sana na unataka kuleta “hijab” ambayo haijasafishwa kwenye ICU!!!

“Ni aina gani ya mawazo ya kipuuzi haya fgs!!!”

Shirika la afya linalojulikana kama Health Simplex liliandika: “Kitengo cha wagonjwa mahututi kinahitaji usafi kabisa kwa sababu wagonjwa walio katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), hasa ‘Watoto Wachanga’ wako hatarini sana.

“Wafanyakazi wa ICU hawaruhusiwi hata kuingia ICU na nguo walizovaa kutoka nyumbani, unadhani kwanini hijabu ingeruhusiwa?”

Wewe unaona kipi ni Sahihi? Tupe Maoni yako hapa kwenye Comment Section…!!!!

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!