Watoto 17,000 wadaiwa kuishi bila Wazazi

Watoto 17,000 wadaiwa kuishi bila Wazazi

Takriban Watoto 17,000 wa Kipalestina na Vijana wamekuwa wakiishi bila wazazi wao au ndugu katika Ukanda Gaza, ambao unakabiliwa na mashambulizi ya Israel tangu Oktoba 7, 2023 kufuatia uvamizi wa Hamas kusini mwa Israel, uliosababisha vifo vya zaidi ya watu 1,200.

Msemaji wa Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa – UNICEF, Jonathan Crickx amesema idadi ya watu waliokufa Gaza imefikia 27,131, wengi wao wakiwa ni Wanawake, watoto au Vijana, huku 66,287 wakijeruhiwa na kwamba Wazazi wa watoto huenda wakawa ama wameuawa, kujeruhiwa au walilazimika kuyahamia maeneo yao.

Naye, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock ameionya Israel dhidi ya kutanua operesheni zake katika mji wa Rafah, kusini mwa Gaza, na kusema hatua hiyo haitakuwa na uhalali wowote akisema Ujerumani na Marekani zimeweka wazi kwa Israel kwamba wakaazi wa Gaza hawawezi kuondoshwa kwenye makaazi yao.

Kauli hiyo, ikekuja kufuatia ripoti zilizomnukuu Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Galant, akisema kwamba watatanua operesheni zao huko Rafah, ili kuzikabili brigedi za Hamas.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!