WHO inasema katika ukanda wa Afrika kuna wavuta sigara milioni 73

WHO inasema katika ukanda wa  Afrika kuna wavuta sigara milioni 73.

Nilivuta sigara tangu mtoto, acheni haina maana- Thierry

Uvutaji wa tumbaku unaunaathiri afya yako.

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, simulizi ya mtu aliyeanza kuvuta sigara akiwa kijana balehe na sasa ameamua kuacha inamulika ni kwa nini shirika la afya duniani(WHO) linasisitiza umuhimu wa kampeni za kuacha tumbaku kwani ni miongoni mwa visababishi vikubwa vya maambukizi ya saratani ya mapafu inayooongoza kwa kuua zaidi vifo miongoni mwa wanaume duniani.

WHO inasema katika ukanda wa  Afrika kuna wavuta sigara milioni 73, na kijana balehe 1 kati ya 10 anavuta sigara. Thierry Anatole kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR sasa mtu mzima alikuwa miongoni mwa takwimu hizo.

Anasema nilivuta sigara kwa miaka 30. Nilianza miaka ya 1980 na nilikuwa na umri wa kati ya miaka 11 na 12. Kwa siku nilikuwa navuta pakiti 4.”

Kwa mujibu wa WHO, nusu ya watu wanaotumia tumbaku, hufariki dunia. Na Tumbaku husababisha aina lukuki za saratani ikiwemo ya mapafu na njia ya hewa.

“Unaweza kuwa na kikohozi mfululizo kwa miezi mitatu, anaendelea Thierry watu wanaweza kukosea na kudhania ni Kifua Kikuu, kumbe ni kikohozi sugu. Na madhara yake ni makubwa.”

Thierry akaendelea kuelezea madhara ya uvutaji kiuchumi akisema “hata wakati wa ukata, huwezi kuacha kuvut

a sigara. Hata kama ni fedha ya kununulia dawa, unanunulia sigara.”

Sasa Thierry yuko uwanjani anafanya mazoezi kwani miaka 7 iliyopita aliamua kuacha kuvuta sigara. Ari ya kulinda watoto wake dhidi ya moshi wa sigara ikaongezeka, “Nilikuwa ninawaumiza bila kutambua.”

WHO inasema moshi kutoka kwa mvutaji sigara husababisha vifo vya zaidi ya watu milioni 1 kila mwaka kwani huathiri afya ya walio karibu nae.

Hapo ndipo akili ilinirudia na kuanzia Aprili 2016 hadi leo sijavuta tena sigara. Nimetoka kwenye kifungo cha sigara, Niko huru! Sasa niña fedha kwenye mifuko yangu. Ninaweza kufanya michezo, nakimbia, na ninapumua vizuri.”

Thierry akatamatisha na ujumbe.

Kwa wavutaji, na wanaotaka kuvuta, kwa waanzao na wanaovuta mara moja moja, wasikilize sauti ndani ya roho yao inayosema acha kuvuta sigara, usisubiri hadi ukachelewa kwani uvutaji unaua kila siku.”

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!