Breaking: Mfanyabiashara Maarufu Babu Rama Wa Kariakoo Ajiua Kwa Kujipiga Risasi Kichwani
Breaking: Mfanyabiashara Maarufu Babu Rama Wa Kariakoo Ajiua Kwa Kujipiga Risasi Kichwani
Mfanyabishara maarufu wa mikoba katika Mtaa wa Kongo kwenye Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo jijini Dar, Ramadhani Ntunzwe almaarufu Babu Rama anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi ya kichwani .
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa mfanyabishara huyo, tukio hilo limejiri asubuhi ya leo Machi 06, 2024 huko nyumbani kwa mfanyabishara huyo wilayani Urambo Mkoa wa Tabora.
Kwa takribani miaka sita, Babu Rama alilalamika kuhujumiwa na watu kwenye biashara zake ambapo alifikisha malalamiko yake kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kisha kwa Hayati John Pombe Magufuli kabla ya baadaye mwaka 2022 pia kuzungumza kupitia GLOBAL TV akimtaka Rais Samia kuingilia kati sakata lake.
Kuna wakati Babu Rama aliieleza GLOBAL TV kuwa kuna watu walikuwa wanamtishia kumuua na walifanya majaribio kadha wa kadha ya kufanikisha azma yao, lakini walishindwa.
Kuhusu tukio la kujiua kwa kujipiga risasi kichwani, Babu Rama alipokea taarifa za kifo cha kaka yake ndipo akaingia ndani na kujifungia kabla ya kutafutwa na kukutwa akiwa amejiua kwa kujipiga risasi kichwani.
Kwa mujibu wa mfanyabishara mwenzake aitwaye Msifuni, Babu Rama alipata taarifa za kifo cha kaka yake kisha aliingia ndani na kujifungia ndani kabla ya baadaye kugundulika amefikwa na umauti.
Kaka wa marehemu wa Babu Rama amethibitisha kutokea kwa kifo cha kaka yake na namna Polisi walivyofika na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi wa kipolisi na taratibu nyingine.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!