Dalili za ukimwi kwenye uume,Soma hapa kufahamu

Dalili za ukimwi kwenye uume

Dalili za HIV/AIDS kwenye uume zinaweza kujumuisha maumivu, kuwasha, kuvimba, au maambukizi yanayoshindwa kupona. Hata hivyo, dalili hizi pekee hazimaanishi mtu ameambukizwa HIV.

Ni muhimu kufanya vipimo vya HIV ili kuthibitisha hali yako ikiwa una wasiwasi. Kumbuka, dalili zinaweza kutofautiana kati ya watu na hii si njia sahihi ya kutambua ugonjwa huo.

Dalili za ukimwi kwenye uume

Kumbuka; Dalili hizi pekee hazitoshi kusema una maambukizi ya Ukimwi, dalili hizi huweza kuingiliana na matatizo mengine ya kiafya,

Hizi hapa ni baadhi ya Dalili za Ukimwi kwenye Uume;

– Kupata maumivu wakati unafika kileleni(Pain with ejaculation).

– Kupata vidonda kwenye Uume au ngozi ya Uume(Sores or ulcers on the penis).

– Kutokwa na uchafu usio wakawaida kwenye Uume.

– Kupata maumivu ndani ya Uume au kuzunguka Uume

– Kupata maumivu kwenye korodani,au eneo kati ya ngozi ya korodani(Scrotum) na njia ya haja kubwa(anus).

– Kupata shida ya Uume kushindwa kusimama vizuri(Erectile dysfunction). n.k

Dalili za Ukimwi kwa Ujumla

Dalili za HIV/AIDS zinaweza kutofautiana kati ya watu na zinaweza kuchukua muda kidogo kujitokeza baada ya kuambukizwa. Baadhi ya dalili zinazoweza kutokea ni pamoja na:

1. Homa isiyoeleweka:

Homa za mara kwa mara ambazo haziwezi kuelezewa Sababu yake halisi ni nini.

2. Kuhisi uchovu na kukosa nguvu:

Kutokuwa na nguvu na uchovu wa mwili bila sababu za wazi.

3. Kupungua kwa uzito:

Kupoteza uzito bila sababu za msingi.

4. Kuvimba tezi:

Kuvimba kwa tezi za limfu kwenye shingo, kifundo cha mgongo, au sehemu nyingine za mwili.

5. Koo kuwa kavu na kupata maumivu ya koo:

Koo kuwa kavu,hali isiyoisha pamoja na kupata maumivu ya koo yanayodumu, hizi huweza kudalili pia za maambukizi ya VVU

6. Kikohozi kisichoisha:

Kupata Kikohozi kisichoisha, hasa kwa muda mrefu.

7. Kupata Maambukizi ya ngozi na madoa:

Maambukizi kama vile vipele, madoa, au vidonda ambavyo haviponi haraka.

8. Kutokwa na jasho usiku:

Kutokwa na jasho sana usiku, hasa wakati wa kulala.

9. Tatizo la Kuharisha:

Kuharisha sana au matatizo mengine ya utumbo.

10. Kupata Maumivu ya misuli na viungo:

Maumivu ya mara kwa mara ya misuli na viungo bila sababu wazi.n.k

>>Soma Zaidi hapa Dalili za maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU)

Ni muhimu kutambua kwamba dalili hizi pekee hazimaanishi kwamba mtu ameambukizwa HIV, lakini ni vizuri kupata vipimo vya HIV kwa ushauri wa kitaalamu. Kumbuka, watu wengine wanaweza kuishi na HIV bila kuonyesha dalili kwa miaka mingi.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!