Dawa ya Pregabalin inatibu nini na kwa nini inaweza kuwa hatari?

Dawa ya Pregabalin inatibu nini na kwa nini inaweza kuwa hatari?

Dawa ya pregabalin inahusishwa na vifo duniani kote. Watumiaji hununua dawa hiyo, mara nyingi kutoka katika tovuti zisizo rasmi.

Pregabalin ni nini na inatumikaje?

Dawa ya pregabalin hutumiwa kutibu magonjwa ikiwa ni pamoja na kifafa, maumivu ya neva na wasiwasi.

Inatengenezwa kama vidonge au maji, na inaweza kuitwa Alzain, Axalid, Lyrica au Signature, kulingana na mtengenezaji.

Je,Dawa ya Pregabalin ina madhara gani?

Wengine huiita Valium au Bud (Budweiser) kwa sababu inaweza kuwafanya watumiaji wahisi wametulia, kwa njia sawa na dawa za kutuliza au pombe.

Kuitumia kupita kiasi – haswa ikichanganywa na dawa nyingine za mitaani ambazo pia zina athari – kunaweza kusababisha kusinzia pamoja na shida ya kupumua.

Wagonjwa ambao wameagizwa kutumia pregabalin wanashauriwa kuepuka unywaji wa pombe.

Utegemezi wa pregabalin ni hatari hasa kwa wale walio na historia ya awali ya matumizi mabaya ya dawa za kulevya au uraibu.

Baadhi ya watu hupata ugumu kuacha kutumia pregabalin. Ukitaka kuachana na uraibu wa dawa hii unaweza kupata mabadiliko ya hisia kama vile hasira na kuwashwa, wasiwasi na woga pamoja na dalili za kimwili kama vile kutokwa na jasho, kichefuchefu na baridi.

Historia ya dawa hii ya Pregabalin

Pregabalin ilianzishwa nchini Marekani na Uingereza mwaka 1993.

Yeyote anayejaribu kuacha kutumia dawa hiyo anapaswa kutafuta ushauri wa kiafya kwanza.

Hupaswi kuacha ghafla kutumia pregabalin isipokuwa uache baada ya ushauri wa daktari. Dozi hupunguzwa kwa wiki moja au zaidi.

Katika nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Uingereza kumiliki dawa hii bila sababu halali ya kimatibabu ni kosa la jinai.

Hata hivyo dawa hiyo inauzwa katika maduka ya dawa katika nchi kadhaa za Mashariki ya Kati, na pia katika majimbo mengi nchini India.

Utafiti uliochapishwa na jarida la matibabu la Nature Communications unakadiria kuwa idadi ya dozi za pregabalin zinazotumika kila siku duniani kote iliongezeka zaidi ya mara nne kati ya 2008 na 2018.

Zaidi ya maagizo milioni nane ya pregabalin yalitolewa nchini Uingereza mwaka wa 2022. Mwaka huo, kulikuwa na vifo 441 vilivyoripotiwa kuhusiana na dawa hiyo nchini Uingereza na Wales.

Mwaka 2023, ripoti ya Kila mwaka ya Overdose ya Australia iligundua vifo 887 vilivyohusishwa na pregabalin kati ya 2000 na 2021 – 93% vinahusishwa na pregabalin.

Rekodi kutoka Uingereza zinaonyesha vifo vingi kati ya 2004 na 2020 vinavyohusishwa na pregabalin vilitokea wakati ilipotumika pamoja na dawa nyingine kama vile methadone au morphine.

Matumizi ya pregabalin na gabapentin nchini Serbia yaliongezeka kwa 60% kila mwaka kati ya 2008 na 2018.

Kulingana na data kutoka Kituo chake cha Kitaifa cha Kudhibiti Sumu, watu 374 walikuwa na sumu kali kutokana na dawa hizi kati ya 2012 na 2022. Kati ya 96% walikuwa wametumia pregabalin.

Ripoti rasmi zinaonyesha kuwa dawa hiyo pia inazidi kutumiwa nchini Saudi Arabia na Jordan, hasa na vijana wa kiume.

Mwaka 2017, Kituo cha Kitaifa cha Kurekebisha Tabia cha Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kilisema pregabalin na gabapentin ndizo dawa zinazotumiwa vibaya zaidi na walio na umri wa chini ya miaka 30.

Mwezi Machi, tembe milioni 2.75 zilinaswa kutoka genge la wasafirishaji huko UAE.

Mwaka 2023, mamlaka nchini Kuwait ilikamata vidonge milioni 15 vya pregabalin na nusu ya tani ya dawa hiyo ikiwa katika hali ya unga.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!