Huduma ya upimaji na uchunguzi wa Magonjwa ya Macho, masikio, saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti

Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, tarehe 8 Machi ,2024

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imeendesha huduma ya upimaji na uchunguzi wa Magonjwa ya Macho, masikio, saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza lengo likiwa ni kuwafikia wananchi ambao wanashindwa kufika hospitali kwa sababu mbalimbali.

huduma hii ambayo inaratibiwa na Wanawake wa Bugando ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani inafanyika kwa siku tatu mfululizo, tarehe 04 – 06, Machi 2024 katika maeneo ya Bujingwa Shule ya Sekondari, Buswelu round about na Mabatini.

Akizungumzia huduma hii, Mwenyekiti wa Wanawake Bugando Bi. Eunice Kitula amesema

“wanawake wa Bugando kwa kutambua kuwa jamii hususani wanawake wanakabiliwa na magonjwa mbalimbal ikiwemo kansa ya mlango wa kizazi na Kansa ya matiti na kwa bahati mbaya wengi wetu hatuna utaratibu wa kuchunguza afya zetu mara kwa mara, hali hii imetusukuma kuendesha huduma hii ili kubaini changamoto zozote za kiafya mapema na kuzipatia ufumbuzi kwa kuzitibu na kutoa ushauri wa kitaalamu na ndicho tunachokifanya ” amesema Bi. Eunice Kitula na kuwakaribisha wananchi kujitokeza na kutumia fursa hii adhimu.

Kwa upande wake mtaalamu wa uoni Idara ya Macho Bw. Justice Daffa ametanabaisha kuwa sehemu kubwa kubwa ya wagonjwa waliowaona wana tatizo la uoni hafifu unaotokana na kurithi na wengine wachache umetokana na kujiumiza na vitu mbalimbali ikiwemo vijiti au peni. Bw. Daffa amesiaitiza Wazazi na Walimu kushirikiana kutambua tatizo la uoni hafifu mapema na kalipatia ufumbuzi mapema ili kuepukana na upofu unaoweza kuzuilika na kuongeza kuwa ni rahisi Mwalimu kugundua tatizo la uoni kwa kumwangalia Mwanafunzi kushindwa kuona ubaoni akiwa mbali au akiwa karibu.
@wizara_afyatz
@kanisa_katolikitz
@dr.fabian_massaga

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!