Ticker

6/recent/ticker-posts

Je, Visigino Vyako Vina shida? unapata maumivu au tatizo lolote?



Je, Visigino Vyako Vina shida? unapata maumivu au tatizo lolote?

Matatizo ya kisigino ni ya kawaida na yanaweza kusababisha maumivu. Hii hutokana na mkazo mwingi kwenye mfupa wa kisigino chako na tishu zinazozunguka.

Zipo sababu mbali mbali za kupata tatizo la kisigino ambalo huleta maumivu. Hali hii Inaweza kusababishwa na:

• Majeraha
• Michubuko kutokana na kukimbia au kuruka
• Kuvaa viatu ambavyo havilingani na miguu yako
• Kuwa na uzito kupita kiasi.n.k

Hizi zinaweza kusababisha tendinitis, bursitis, na fasciitis, ambayo ni aina zote za kuvimba kwa tishu zinazozunguka kisigino chako.

Baada ya muda mkazo unaweza kusababisha tatizo la mfupa na ulemavu. Magonjwa fulani, kama vile rheumatoid arthritis, na gout, yanaweza pia kusababisha matatizo ya kisigino.
Matibabu ya matatizo ya kisigino yanaweza kujumuisha:

• Kupumzika
• Dawa
• Mazoezi
• Kuvaa viatu maalum
• Upasuaji hauhitajiki sana.

Kwa Maelezo zaidi:endelea kufuatilia hapa hapa Instagram au, Link google: afyaclass….!!!!!



Post a Comment

0 Comments