kijana Ramadhan Hassan (18) kutoka Tanga apate matibabu bure ya ugonjwa alionao

kijana Ramadhan Hassan (18) kutoka Tanga apate matibabu bure ya ugonjwa alionao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza kijana Ramadhan Hassan (18) kutoka Tanga apate matibabu bure ya ugonjwa alionao katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Rais Samia ametoa maelekezo hayo kufuatia habari iliyorushwa na Globaltvonline ikimuonyesha Ramadhan akihitaji msaada wa matibabu.

Bi. Prisca Manfredi ambaye ni mlezi wa Ramadhani amesema kuwa kijana huyo alisafiri peke yake kutoka Tanga bila ya kuwa na mwangalizi kutokana na ukosefu wa fedha na sasa hupo Mkoa wa Pwani kwa ajili ya matibabu lakini hali imekuwa ngumu kutokana na wao kusosa fedha za matibabu hivyo wanahitaji msaada wa matibabu.

Tunaipongeza Global Tv kwa kuibua habari hii kuhusu kijana huyu mweney uhitaji wa matibabu na sasa Ramadhani Hassan atasafirishwa kuelekea Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi na matibabu bure kwa ugonjwa alionao huku gharama za matibabu yake zitalipwa na Wizara ya Afya.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!