Kipa wa zamani wa Super Falcons, Bidemi Aluko-Olaseni, afariki dunia baada ya kuugua saratani
Kipa wa zamani wa Super Falcons, Bidemi Aluko-Olaseni, afariki dunia baada ya kuugua saratani.
Kipa wa zamani wa Super Falcons ya nchini Nigeria, Bidemi Aluko-Olaseni, amefariki dunia baada ya kuugua saratani ya matiti kwa miaka nane.
Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) lilithibitisha habari hizo za kusikitisha kwenye mtandao wao wa X siku ya Jumamosi.
“Tunasikitika kusikia kifo cha
Golikipa wa Zamani wa Super Falcons, Bidemi Aluko-Olaseni baada ya mapambano ya miaka nane dhidi ya saratani,” NFF iliandika.
“Mawazo na sala zetu ziko pamoja na familia. Roho yake ipumzike kwa amani.”
Awali Aluko aligunduliwa kuwa na saratani ya matiti mnamo Aprili 2017 na alipewa matibabu kamili mwaka mmoja baadaye baada ya kufanyiwa matibabu na upasuaji wa tumbo.
Walakini, aligunduliwa tena na ugonjwa huo mnamo Januari 2019 na alipata Sessions 10 za chemotherapy.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!