Mama ashtakiwa kwa mauaji ya mtoto wake wa miaka mitatu, afukuza timu yake ya wanasheria wakati wa kesi.
Mama mmoja raia wa Uingereza anayedaiwa kumuua mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu amewafuta kazi wanasheria wake baada ya kutoa ushahidi wakati wa kesi.
Christina Robinson anakabiliwa na kesi katika Mahakama ya Taji ya Newcastle akishtakiwa kwa kumchoma, kumpiga viboko na kumuua mwanawe, Dwelaniyah, nyumbani kwao eneo la County ya Durham,
Mwanamke huyo amekanusha mauaji na ukatili huo wa mtoto.
Robinson alitoa ushahidi Jumatano na Alhamisi akikana kumtikisa mtoto huyo hadi kufa au kumchoma kwa makusudi kwa kumweka kwenye maji ya moto.
Kulingana na Mail Online, kesi hiyo ilipaswa kuendeshwa katika hatua inayofuata siku ya Ijumaa lakini haikufanyika baada ya kuamua kutupilia mbali huduma za mawakili wake.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!