Mtindo bora wa maisha huepusha hatari ya Magonjwa ya Figo

Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe. Kanali Maulid Hassan Surumbu ameongoza katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani, Mkoani Mara katika Viwanja vya Mukendo Tarehe 14 Machi 2024 akimwakilisha Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu.

Katika Maadhimisho hayo jamii imekumbushwa kufuata mtindo bora wa maisha ikiewemo kufanya mazoezi, kuepuka matumizi ya tumbaku, kuepuka tabia ya kuvuta sigara au bidhaa yoyote ya tumbaku huku akikumbushia umuhimu wa kuchunguza afya mara kwa mara kwani Mtu ni Afya.

Elimu ya Afya pamoja na huduma mbalimbali za Afya ikiwemo upimaji wa Shinikizo la juu la damu,uwiano wa urefu na uzito zimefanyika katika maadhimisho hayo ambapo kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wananchi.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!