Polisi waokoa watoto 251 katika dhehebu tata nchini Zimbabwe.
Watoto waliookolewa “walikuwa wakitumiwa kufanya shughuli mbalimbali kwa manufaa ya kiongozi wa dhehebu”, taarifa ya polisi ilisema.
–
Polisi walisema wengi wa watoto hao 251 waliopatikana katika shamba la Ishmael Chokurongerwa, 56 huko Nyabira, hawakuwa na vyeti vya kuzaliwa na hawakuruhusiwa kuhudhuria shule.
–
Polisi pia waligundua kaburi katika shamba hilo ambapo watu 16 wamezikwa kwa siri, wakiwemo watoto wachanga saba.
–
Mmoja wa washiriki wa madhehebu hayo aliwaambia waandishi kwamba elimu rasmi shuleni haitakiwi na Mungu “kwa sababu ni kinyume na mafundisho ya Mungu”.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!