Sita wakimbizwa hospitalini kwa kula chakula chenye Sumu Gerezani.
Watu sita wamekimbizwa hospitalini baada ya kula mlo mmoja katika gereza la Lewes huko Sussex, Uingereza.
Kwa sasa, hakuna hata mmoja wa wale waliokimbizwa hospitalini anayefahamika kuwa katika hali ya kutishia maisha au mgonjwa sana.
Taarifa zinasema; wafanyakazi watatu na wafungwa watatu walipelekwa katika Hospitali ya Kaunti ya Royal Sussex huko Brighton.
Msemaji wa Jeshi la Magereza alisema: “Tunafanya kazi na huduma za dharura kushughulikia tukio linaloshukiwa kuwa la sumu ya chakula huko HMP Lewes.”
Ambulensi ya Pwani ya Kusini Mashariki ilithibitisha kwa The Sun kuwa walikuwa gerezani. Msemaji alisema: “Tunaweza kuthibitisha kuwa tunahudhuria tukio huko HMP Lewes lililoripotiwa kwetu takriban adhuhuri leo.”
Polisi wa Sussex pia walithibitisha walikuwa wakisaidia huduma ya ambulensi “kufuatia ripoti ya tukio la matibabu huko HMP Lewes karibu 12.30pm.”
HMP Lewes inaweza kuwaweka wafungwa 624 katika seli moja na mbili, Na ilifunguliwa mwaka wa 1853. Kama gereza la kitengo B, inawashikilia wafungwa waliochukuliwa moja kwa moja kutoka mahakama za Kent, Surrey, na Sussex.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!