Vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga vimepungua na kufikia 104 katika kila vizazi hai laki moja

Vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga vimepungua na kufikia 104 katika kila vizazi hai laki moja.

“Vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga vimepungua na kufikia 104 katika kila vizazi hai laki moja hii ni kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa ndani ya Miaka 3 ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujenga miundombinu tiba, vifaa tiba, kuongeza watumishi na madawa” amesema Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya kurasa 365 za Mama, Jijini Dar Es Salaam Machi, 13, 2024

Kampeni yenye lengo la kuyamulika maendeleo yalifanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kipindi cha Miaka 3 ya uongoziwa wake wa Serikali ya awamu ya Sita

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!