Visa vya vifo vinavyohusiana na joto kupita kiasi vyaripotiwa

Visa vya vifo vinavyohusiana na joto kupita kiasi vyaripotiwa.

Joto kali lasababisha shule kufungwa Sudan kusini.

“Tayari kuna visa vya vifo vinavyohusiana na joto kupita kiasi vinavyoripotiwa,” mamlaka ilisema katika taarifa yake.

Serikali ya Sudan Kusini imeamuru kufungwa kwa shule zote kwa muda usiojulikana kwa sababu ya wimbi la joto ambalo linaweza kusababisha joto kuongezeka hadi 45C (113F).

Mamlaka ya afya na elimu pia iliwataka wazazi kuwazuia watoto wao kucheza nje kwa muda mrefu, wakisema joto hilo linaweza kudumu kwa wiki mbili.

Wiki iliyopita, takriban watoto 15 waliripotiwa kufariki kutokana na homa ya uti wa mgongo na magonjwa mengine yanayohusiana na joto, kulingana na wizara ya afya.

Via:bbcswahili

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!