Fahamu Matumizi ya Hemovit Syrup
Hemovit Syrup; Hii ni dawa ya kuongeza damu ambayo hutumiwa sana na Wakina mama wajawazito wenye tatizo la Upungufu wa damu,
Tuichambue dawa hii ya Hemovit kwa kina hapa kwenye Makala hii;
HEMOVIT
Huu ndyo mchanganyiko wa dawa hii,
Generic name; Iron,Zinc,Vitamins and Folic acid capsules and syrup with Iron,Zinc,Vitamin B6,Vitamin B12 and folic acid.
Dawa hii inakuwa kwenye form mbili(Dosage form);
- Kuna Syrup ambayo hujulikana kama Hemovit syrup
- Na Tembe/vidonge au Capsules
Njia ya kuitumia au kwa kitaalam; Route of administration; Ni kupitia Mdomoni(Oral)
Vitu vinavyounda Dawa hii(Content of active Ingredients)
Hivi ni vitu vinavyounda dawa hii ya Hemovit, dawa kwa ajili ya kuongeza damu
(a) Kila kidonge kimoja(Capsule) kina;
- Ferrous Fumarate BP equivalent to elemental Iron 100mg
- Ascorbic acid BP (Vitamin C) 75mg
- Folic acid BP 0.75mg
- Cyanocobalamin Bp (Vitamin B12) 5mcg
- Zinc Sulphate Bp 5mg
(b) Kila 5mls za Hemovit Syrup zina;
- Ferric Ammonium Citrate Bp 200mg(equivalent to elemental Iron 43mg)
- Folic acid Bp 1.50mg
- Pyridoxine Hydrochloride Bp (Vitamin B6) 0.5mg
- Cyanocobalamin Bp (Vitamin B12) 50mcg
- Zinc Sulphate Bp (equivalent to elemental Zinc 0.53mg) 2.33mg
Matumizi ya Dawa hii ya Hemovit
Dawa hii hutumika kama una tatizo la upungufu wa damu yaani Iron deficiency anemia, au kama njia ya kukukinga Usiingie kwenye tatizo hili(prophylaxis),
Dawa hii huweza kutumika kwa;
- Wajawazito
- Wakina mama wanaonyonyesha
- Watoto wanaokua n.k
Doses Zake kulingana na Umri
(1) Vidonge(Capsules)
– Watoto; Kidonge kimoja(1) kila siku
– Watu Wazima; Vidonge 1-2 kwa siku
(2) Hemovit Syrup
– Watoto(umri miaka 2-6); Kijiko kimoja(1) sawa na 5mls mara mbili kwa siku
– Watu Wazima; Vijiko 2 sawa na 10mls mara 3 kwa siku.
Maudhi madogo madogo ya dawa hii(Side Effects)
1. Kukusababishia shida ya kuharisha
2. Kupata Maumivu ya Tumbo
3. Kuhisi kichefuchefu na kutapika n.k
• Usitumie dawa hii endapo, unachangiwa damu mara kwa mara(Patients receiving repeated blood transfussions)
• Au Upungufu wako wa Damu haujatokana na Upungufu wa madini chuma(Iron deficiency anemia)
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!