Fahamu Vyakula vya kula wakati wa maandalizi ya kubeba ujauzito
Fahamu Vyakula vya kula wakati wa maandalizi ya kubeba ujauzito
Yapo maandalizi mbalimbali ambayo wenza wanaokusudia kutafuta ujauzito wanapaswa kuyafanya. Miongoni mwa maandalizi hayo ni kuwa na lishe bora yenye virutubishi kutoka katika makundi yote ya vyakula.Mlo kamili husaidia kuuandaa mwili kuwa katika hali nzuri ya kutungisha na kuutunza ujauzito.
Umuhimu wa chakula katika mandalizi ya ujauzito
Zifuatazo ni faida za mlo kamili katika kipindi cha maandalizi ya kupata ujauzito kwa mwanamke na mwanaume;
– Kupata virutubishi ambavyo husaidia mwili kufanya kazi vema na kuimarisha afya ya uzazi
– Kusaidia kuongeza ubora wa mbegu za kiume na uovuleshaji
– Kupunguza msongo katika mwili unaoweza kuathiri afya ya uzazi
– Kuzuia mtoto kuzaliwa na kasoro za kimaumbile, mfano matumizi ya vyakula vyenye madini ya folate (foliki asidi)
– Kuzuia upungufu wa damu katika kipindi cha ujauzito, mfano vyakula vyenye madini chuma
– Kuufanya mwili uwe katika uzito unaoshauriwa kiafya, ambao una athari chanya katika afya ya uzazi
Vyakula unavyoshauriwa kutumia kwa wingi
Unashauriwa kutumia vyakula vifuatavyo kwa wingi unapokuwa katika maandalizi ya kutafuta ujauzito;
1. Vyakula vyenye madini ya zinki;
Mfano wa vyakula hivi ni;
- nyama,
- mimea jamii ya kunde ,
- nafaka zisizokobolewa,
- mbegu, karanga nk
2. Vyakula vyenye madini ya folate (foliki aside);
Mfano wa vyakula hivi ni maini, mayai, mboga za majani za kijani nk
3. Vyakula vyenye vitamini hasa vitamin C;
Mfano wa vyakula hivi ni; atunda jamii ya limao, mboga za majani, mbegu nk
4. Vyakula vyenye madini chuma;
Mfano wa vyakula hivi ni nyama, spinachi, maharagwe nk
5. Vyakula vyenye nyuzi nyuzi;
Mfano wa vyakula hivi ni nafaka zisizokobolewa, mboga za majani, matunda nk
Vyakula ambavyo hupaswi kutumia
Matumizi vyakula hivi kwa wingi huathiri afya ya uzazi:
- Vyakula vya kusindika
- Nafaka za kukobolewa
- Vinywaji vyenye sukari nyingi
- Vyakula vyenye mafuta mengi
- Pombe
Wapi utapata maelezo zaidi
Kwa maelezo zaidi kuhusu maandalizi ya kufanya wakati wa kutafuta ujauzito bofya hapa;
Rejea za Mada;..
Female Fertility and the Nutritional Approach: The Most Essential Aspects – NCBI. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC8634384/. Imechukuliwa 19.02.2024
Diet and Nutritional Factors in Male (In) fertility—Underestimated Factors. NCBI. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7291266/. Imechukuliwa 19.02.2024
16 Natural Ways to Boost Fertility – Healthline. https://www.healthline.com/nutrition/16-fertility-tips-to-get-pregnant. Imechukuliwa 19.02.2024
The Influence of Metabolic Factors and Diet on Fertility – PMC. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC10005661/. Imechukuliwa 19.02.2024
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!