Hii ni mikoa 10 inayoongoza kwa uzazi wa mpango Tanzania

Hii ni mikoa 10 inayoongoza kwa uzazi wa mpango Tanzania

Miongoni mwa masuala yanayogusa zaidi vijana wengi waliopo kwenye ndoa na wasio kwenye ndoa kwa sasa ni suala la kuwa na watoto.

Miongoni mwa maswali makubwa huwa ni lini wapate watoto, idadi ya watoto lakini ni njia gani sahihi itakayomfanya wanawake vijana wasipate ujauzito bila kutarajia. Wataalamu wanasisitiza kuwa ni vema wazazi vijana wakapanga mipango yao vema ya kijamii na kiuchumi kabla ya kupata watoto.

Hata hivyo, si watu wote wanapanga ipasavyo juu ya kupata watoto. Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa mwaka 2022 unabainisha kuwa nchini Tanzania takriban wanawake wanne kati ya 10 au asilimia 38 ya waliolewa wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wanatumia njia ya aina yeyote ya uzazi wa mpango.

Ripoti ya utafiti huo uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa ushirikiano na taasisi nyingine iwepo Wizara ya Afya inabainisha ipo baadhi ya mikoa yenye kiwango kikubwa cha wanawake wenye wanaotumia ipasavyo njia za uzazi wa mpango ikiongozwa na Njombe huku mingine ikitumia kwa kiwango kidogo sana kama Simiyu.

Je, waifahamu mikoa inayoongoza kwa matumizi ya njia za uzazi wa mpango Tanzania?

Rejea Source Links;

Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa mwaka 2022

Ripoti ya utafiti huo uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)

Wizara ya Afya

• Nukta Page

>>Soma pia kuhusu Njia Mpya ya Uzazi wa mpango inayojulikana kama SAYANA PRESS

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!