Josphine kutoka Kenya anaishi na hali inayoathiri ubongo ‘Cerebral palsy’ kwa kiingereza

Josphine Mwende, mwenye umri wa miaka 34, kutoka Kenya anaishi na hali inayoathiri ubongo ‘Cerebral palsy’ kwa kiingereza.

Anasema moja ya changamoto alizokabiliana nazo ilikuwa ni ulimwengu wa kupata mpenzi na kuolewa.

“Nilihisi kana kwamba watu walikuwa wakidhani kwamba mtu kama mimi sipaswi kujihusisha na mapenzi ila hali halisi ni kuwa, hata sisi tunahisia kama watu wengine,”

Miaka nane iliyopita aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mmoja lakini alipogundua ameshika ujauzito mpenzi wake alipotea na hakuonekana tena.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!