Kenya yarejesha dawa ya kikohozi ya watoto ya kampuni ya Johnson & Johnson
Kenya yarejesha dawa ya kikohozi ya watoto ya kampuni ya Johnson & Johnson.
Mamlaka ya kudhibiti viwango vya dawa nchini Kenya imeamuru kurejeshwa kwa dawa ya kikohozi ya watoto ya kampuni ya Johnson & Johnson.
Hatua hiyo imechukuliwa siku moja tu baada ya Nigeria kuamuru kurejeshwa kwa dawa hiyo ya Benylin Paedriatic. Idara ya afya nchini Nigeria ilisema vipimo vya maabara vya dawa hiyo ya maji vilionyesha kiwango kikubwa cha aina ya kemikali inayohusishwa na vifo vya makumi ya watoto nchini Gambia, Uzbekistan na Cameroon tangu mwaka wa 2002.
Bodi ya Dawa na Sumu nchini Kenya – PPB imesema katika taarifa kuwa imeanzisha uchunguzi na kushauri kuwa mauzo ya baadhi ya dawa hizo yasitishwe na kurejeshwa kwa wanaozisambaza. Kampuni ya Kenvue, ambayo sasa inamiliki chapa ya Benylin baada ya kuuzwa kutoka kampuni mama ya J&J mwaka jana, haijajibu mara moja ombi la kutaka kauli yake.
Bodi ya PPB imesema dawa zinazorejeshwa zilitengenezwa na kampuni ya J&J nchini Afrika Kusini mnamo Mei 2021 na muda wake wa matumizi unamalizika Aprili 2024.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!