kujiepusha na maradhi yatokanayo na mifumo mibovu ya ulaji chakula-Prof Janabi

kujiepusha na maradhi yatokanayo na mifumo mibovu ya ulaji chakula-Prof Janabi

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amewataka watu kuendeleza na mtindo wa kula waliokuwa wakiufuata katika kipindi cha kufunga hata baada ya kipindi cha mfungo wa kwaresma na Ramadhani kuisha ili kuimarisha afya zao na kujiepusha na maradhi yatokanayo na mifumo mibovu ya ulaji chakula.

Wakati Waislam kote ulimwenguni wakisheherekea sikukuu ya EId El Fitri Prof. Janabi akifanya mahojiano maalumu na EATV anawakumbusha watu kuhusu mpangilio mzuri wa ulaji vyakula ili kulinda afya zao.

“Kufunga hakutofautiani na maputo tunayoweka, kwa kipindi hiki kwa kupenda au kutokupenda tumeingia kwenye kula milo miwili, hii inasaidia sana” Prof. Janabi

Aidha Prof. Janabi amewakumbusha wahudumu wa afya kuwa jukumu lao sio kutibu tu maradhi ya watu bali pia kupunguza watu wenye magonjwa kwa kuwahimizw kujikinga na magonjwa hasa yasiyo ya kuambukizwa.

“Kinga ni bora zaidi kuliko kusubiri mpaka magonjwa yatokee, mtu anapokuja kwetu na matatizo ya moyo, saratani na mengine, tunajuuliza ni nini sisi tumefanya kama madaktari kumkinga” amesema Prof. Janabi

Na hapa baadhi ya wananchi wanaeleza kuwa wakati mwingine wamekuwa wakishindwa kumudu kula mlo kamili kutokana na hali zao za kiuchumi kuwa duni.

“Tunakula vyakula ambavyo vina kemikali nyingi sana, kwa mafano hizi ‘energy’ tunaambiwa zinachangia kwenye magonjwa ya presha” Amesema Amani

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!