Oedema ni ugonjwa gani,Fahamu kuhusu tatizo hili
Oedema au “Edema ni mrundikano wa maji mwilini ambayo husababisha tishu zilizoathirika kuvimba. Uvimbe huo unaweza kutokea katika sehemu fulani ya mwili au mwili wote kwa ujumla kulingana na sababu.
Kama una Uvimbe ambao hauishi wenyewe hakikisha unawaona wataalam wa afya.
Dalili za Oedema
Mkusanyiko wa maji chini ya ngozi husababisha uvimbe. Hali hii mara nyingi hutokea kwenye miguu na vifundoni(ankles)
Pamoja na uvimbe huu wa ngozi, ikiwa una uvimbe, unaweza pia kupata dalili nyingine ikiwa ni pamoja na:
- kubadilika rangi ya ngozi(skin discolouration)
- Eneo la ngozi kutengeneza kishimo kwa muda baada ya kubonyeza na kidole(Tazama picha) (pitting oedema)
- kupata maumivu pamoja na viungo kuwa laini
- Kukakamaa kwa joints
- Uzito kuongezeka Zaidi n.k
Chanzo cha oedema
Wakati mwingine Si dalili ya ugonjwa kupata uvimbe kwenye miguu, Hali Hii inaweza kutokea hasa ikiwa umekaa au umesimama kwa muda mrefu.
Edema kidogo ni ya kawaida katika ujauzito, na sio kitu cha kuwa na wasiwasi. Fahamu pia Edema inaweza kuwa dalili na Ishara ya hali flani ya kiafya, haswa ikiwa uvimbe ni wa muda mrefu au kudumu, au kuna dalili zingine muhimu (kama vile upungufu wa damu, shida ya kupumua)n.k.
Oedema inaweza kutokea kama matokeo ya matatizo ya kiafya kama vile:
– Tatizo la Moyo kushindwa kufanya kazi
– Ugonjwa sugu wa mapafu
– Ugonjwa wa tezi
– Au matumizi ya dawa, kama vile dawa jamii ya corticosteroids au dawa ya shinikizo la juu la damu (shinikizo la damu)
– Kutumia Vidonge vya kuzuia mimba
– Kutoweza kutembea kwa Muda mrefu
– Kukaa kwa muda mrefu au kusimama kwa muda mrefu ni miongoni mwa sababu inayojulikana zaidi ya uvimbe kwenye miguu.
Sababu zingine zinazowezekana ni pamoja na:
- kuganda kwa damu
- kuwa na shida kwenye mishipa au tatizo la varicose
- Kupata jeraha la mguu au upasuaji wa mguu
- kuungua kwa ngozi n.k
Ikiwa una hali hii ya Kuvimba hakikisha unafanya Vipimo na kupata Tiba mapema
AU KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!