Suala la kurejesha usimamizi TFDA kwa TMDA bado linaendelea kujadiliwa

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema suala la kurejesha usimamizi TFDA kwa TMDA bado linaendelea kujadiliwa ndani ya Serikali na litakapokamilika mapendekezo ya utekelezaji yatawasilishwa ndani ya Bunge

Dkt. Mollel amebainisha hayo wakati wa Bunge la 12, Mkutano wa 15 na kikao cha tano akijibu swali Namba 58 kutoka kwa Mbunge wa Moshi Mjini Mhe. Priscus Jacob Tarimo aliyetaka kuja Je, upi mpango wa kurejesha TFDA? kwani imeacha masuala ya chakula na inakinzana na utaratibu wa usimamizi wa chakula na madawa duniani?

“Serikali katika kuimarisha mazingira ya kibiashara nchini, ilifanya maamuzi kupitia Bunge lako tukufu ya kuhamisha majukumu ya usimamizi na udhibiti ubora wa chakula na vipodozi kutoka iliyokuwa TFDA na kuyapeleka TBS ambako ndiko afua zote za usimamizi zinatekelezwa huko kwa sasa”, ameeleza Dkt.Mollel

Credits: WizaraafyaTz

REVIEWED BY: @afyaclass

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!