Ugonjwa wa varicocele,chanzo,dalili na Tiba
Varicocele ni nini?
Ugonjwa wa varicocele ni tatizo linalohusisha kuvimba au kuongezeka ukubwa kwa mishipa ya Veins ndani ya kifuko cha korodani.
(enlargement of the veins within the loose bag of skin that holds the testicles (scrotum).
Mishipa hii husafirisha damu iliyopungukiwa na oksijeni kutoka kwenye korodani. Varicocele hutokea wakati damu inapoingia kwenye mishipa badala ya kuzunguka kwa ufanisi nje ya korodani.
Dalili za Tatizo la Varicocele
Ugonjwa wa varicocele kawaida hutokea upande wa kushoto wa korodani na mara nyingi hauonyeshi Ishara au dalili zozote. Na endapo Utaonyesha, Ishara na dalili zinazowezekana zinaweza kujumuisha:
1. Kupata Maumivu
Unaweza kupata Maumivu makali, kuhisi hali ya kuuma au usumbufu ambao hutokea zaidi wakati umesimama au wakati wa mchana,
Kulala chini mara nyingi hupunguza aina hii ya maumivu.
2. Kuhisi kitu kigumu kwenye korodani.
Ikiwa varicocele ni kubwa vya kutosha, kitu kigumu(Mass) kama “mfuko wa minyoo” kinaweza kuonekana juu ya korodani.
Varicocele ndogo inaweza kuwa vigumu sana kuonekana lakini unaweza kuihisi kwa kugusa.
3. Korodani kuwa na Size au ukubwa tofauti.
Ingawa pia kwa kawaida,korodani huweza kutofautiana Size, lakini pia moja ya dalili kwa Mtu mwenye Varicocele ni korodani kuwa na Size tofauti.
Korodani iliyoathiriwa inaweza kuwa ndogo sana kuliko korodani nyingine.
4. Mwanaume kushindwa kumpa mimba mwanamke(Ugumba/Infertility).
Ugonjwa wa varicocele unaweza kusababisha ugumu kwa mwanaume kumpa mwanamke mimba na kuzaa mtoto, lakini sio varicoceles zote husababisha Shida hii ya Infertility.
Hii huweza kuwa dalili na Madhara ya tatizo la Varicocele kwa Mwanaume.
Chanzo cha Tatizo la Varicocele
Korodani hupokea damu iliyojaa oksijeni kutoka kwa ateri mbili za korodani – ateri moja kwa kila upande wa korodani,
Vile vile, pia kuna mishipa miwili ya korodani ambayo husafirisha damu iliyopungua oksijeni kurudi kwenye moyo.
Ndani ya kila upande wa korodani, mtandao wa mishipa midogo ambao kwa kitaalam hujulikana kama (pampiniform plexus) husafirisha damu yenye oksijeni kutoka kwenye korodani hadi kwenye mshipa mkuu wa korodani. Varicocele ni matokeo ya upanuzi wa plexus ya pampiniform.
Sababu halisi ya kutokea kwa tatizo la varicocele haijulikani. Ingawa Sababu moja inayochangia au kuongeza uwezekano wa mwanaume kupata shida ya Varicocele inaweza kuwa kutofanya kazi vizuri kwa vali ndani ya mishipa ambayo inakusudiwa kuweka damu katika mwelekeo unaofaa.
Pia, mshipa wa korodani wa kushoto hufuata njia tofauti kidogo kuliko mshipa wa kulia – njia ambayo hufanya tatizo la mtiririko wa damu kuwa zaidi upande wa kushoto.
Wakati damu iliyopunguzwa oksijeni inapopata nafasi kuingia kwenye mtandao wa mishipa, hupanua na kuunda varicocele.
Matibabu ya Tatizo la Varicocele
Ugonjwa wa varicocele mara nyingi hauhitaji kutibiwa. Kwa mwanamume aliye na shida ya kushindwa kumpa mwanamke mimba(Infertility), upasuaji wa kurekebisha varicocele unaweza kuwa sehemu ya mpango wa matibabu ili kurudisha uwezo wa kumpa mwanamke mimba.
Kwa vijana au Watu wazima – kwa ujumla wale ambao hawatafuti matibabu ya uzazi – mtoa huduma wa afya anaweza kupendekeza uchunguzi wa kila mwaka ili kufuatilia mabadiliko yoyote. Upasuaji unaweza kupendekezwa katika hali zifuatazo:
- Korodani kushindwa kukua
- Kuwa na Idadi ndogo ya manii(Tatizo la Low sperm count) au makosa mengine yanayohusu manii/mbegu za kiume
- Maumivu ya muda mrefu yasiyodhibitiwa na dawa za maumivu
Upasuaji:
Madhumuni ya upasuaji ni kuziba mshipa ulioathiriwa ili kuelekeza mtiririko wa damu kwenye mishipa yenye afya na inayotakiwa. Hili linawezekana kwa sababu mifumo mingine miwili ya ateri-na-Veins hutoa mzunguko wa damu kwenda na kutoka kwenye korodani.
Matokeo ya matibabu haya ya Upasuaji yanaweza kujumuisha yafuatayo:
– Korodani iliyoathiriwa hatimaye inaweza kurudi katika ukubwa wake unaotarajiwa.
– Kwa vijana ambao bado wanakua, Ukuaji wa Korodani unaweza kurudi mahali pake.
– Idadi ya manii inaweza kuongezeka, na hitilafu za manii zinaweza kusahihishwa.
– Upasuaji unaweza kuboresha uwezo wa kushika mimba au kuboresha ubora wa shahawa kwa ajili ya urutubishaji katika mfumo wa uzazi
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
• SOMA pia kuhusu Ugonjwa wa busha kwa Wanaume
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!