Madaktari bingwa wa Rais Samia wamefanikiwa kutoa mawe kwenye kibofu cha mkojo cha Bw. Leonard Mhunda Mkazi wa Chamwino Mkoani Dodoma ambayo yalimtesa kwa takriban miaka 10.
Akizungumza mara baada ya kumfanyia upasuaji na kumtolea Mawe kwenye kibofu Daktari Bingwa wa upasuaji Dkt. Tito Lyimo amesema mgonjwa huyo alifika hospitalini hapo Tarehe 13, Mei 2024 na kufanikiwa Kufanyiwa upasuaji tarehe 15 Mei 2024 na kutoa mawe hayo.
“Tumefanikiwa kuwafanyia wagonjwa wanne upasuaji mgonjwa wa kwanza ni mgonjwa aliekua na goiter ambao haitoi kichocheo, wapili alikua na mawe kwenye kibofu cha mkojo” amesema Dkt. Tito
Kwa upande wake Bw. Leonard Mhunda amewashukuru Madaktari Bingwa na Bobezi katika Hospitali ya Wilaya ya Chamwino baada yakufanikisha kumtolea mawe kwenye Kibofu.
Bw. Leonard, amesema mara baada yakusikia tangazo la ujio wa madaktari Bingwa na Bobezi ilimlazimu kuchukua hatua kwenda Hospitali ya Wilaya ya Chamwino kwa ajili yakuwaona wataalam hao, ambapo ndugu yake alimpeleka kwa ajili ya matibabu.
Bw. Leonard amesema tatizo lake lilianza miaka kumi iliyopita, lakini hakuweza kwenda hospitalini akiamini huenda mara baada yakutumia dawa ya Mganga wa kienyeji angeweza kupona.
Bw. Leonard ametumia fursa hiyo, kuiasa jamii kuepukana na mila potofu na badala yake wakipata changamoto wafike katika vituo vya kutolea huduma za afya na kukutana na wataalam wa afya pamoja na kupima afya zao mara kwa mara.
Hata hivyo, ndugu wa Bw. Leonard, wameishukuru Serikali kwa ujio wa Madaktari Bingwa kusogezwa karibu na wananchi huku wakiiomba iwe ni zoezi endelevu.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!