ASILIMIA 77.5 YA KAYA ZOTE NCHINI ZINATUMIA VYOO BORA
Kaya zenye vyoo bora zimeongezeka hadi kufikia kaya 7,775,181 ikiwa ni sawa na asilimia 77.5 katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi, 2024 ukilinganisha na kaya 7,087,523 sawa na asilimia 73.2 zilizokuwa na vyoo bora katika kipindi kama hicho mwaka 2022/23.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu tarehe 13 Mei, 2024 wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Afya mbele ya Bunge la Bajeti la 12, Mkutano wa 15, Kikao cha 24 Jijini Dodoma.
Mhe. Ummy amesema ongezeko la kaya 687,658 sawa na asilimia 4.3 katika kipindi cha mwaka mmoja ambapo Lengo la Wizara ni kufikia asilimia 85 ifikapo mwaka 2025 na kuongeza kuwa jitihada zinaendelea ili kuweza kufikia shabaha iliyojiwekea.
Ameeleza kuwa Katika kutekeleza azma ya kuboresha matumizia ya vyoo bora, Wizara kwa kushirikiana na Mikoa na Halmashauri inaendelea kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa afua za Afya Mazingira na Usafi katika Mikoa yote ya Tanzania Bara.
Mwisho.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!