Connect with us

Magonjwa

Chuchu kutoa maziwa ni dalili ya nini

Avatar photo

Published

on

Chuchu kutoa maziwa ni dalili ya nini

Chuchu kutoa maziwa inaweza kuwa dalili ya ujauzito au inaweza kutokea kwa sababu ya mabadiliko ya homoni au matibabu fulani. Katika Makala hii tunajadili tatizo la chuchu kutoa Maziwa yenyewe au maji maji wakati sio mjamzito wala hunyonyeshi.

CHUCHU KUTOA MAZIWA YENYEWE AU MAJIMAJI

Chuchu kutoa maziwa yenyewe wakati wewe sio Mjamzito wala hunyonyeshi,
Hili ni tatizo na linawasumbua wanawake wengi siku hizi. Wengi wao wakijiuliza hivi hii ni nini na ina maana Gani?. Je ni kansa ya titi au nini?

Chuchu Kutoa Maziwa yenyewe au majimaji

Galactorrhea ni tatizo la Chuchu Kutoa Maziwa yenyewe hali ambayo ni tofauti na maziwa yakawaida yanayotoka wakati wa unyonyeshaji,

Galactorrhea sio ugonjwa bali huweza kuwa dalili za ugonjwa flani.

Mara nyingi tatizo hili hutokea kwa wanawake hata kama hujawa na mtoto,hunyonyeshi na hata baada ya kufikia kipindi cha Ukomo wa hedhi(menopause). Lakini pia galactorrhea huweza kutokea hata kwa wanaume na watoto pia.

Kusisimuliwa kwa matiti kupita kiasi, madhara ya dawa au matatizo ya tezi ya pituitari yote yanaweza kuchangia tatizo la Chuchu Kutoa Maziwa yenyewe(galactorrhea). Mara nyingi, matokeo ya galactorrhea hutokana na kuongezeka kwa viwango vya prolactini, homoni ambayo huchochea uzalishaji wa maziwa.

Wakati mwingine, sababu ya moja kwa moja ya tatizo la Chuchu Kutoa Maziwa yenyewe(galactorrhea) haijulikani. Na Hali hii inaweza kuisha peke yake pasipo matibabu yoyote.

Dalili za tatizo la Chuchu Kutoa Maziwa yenyewe(galactorrhea)

Hizi hapa ni baadhi ya dalili za tatizo la chuchu kutoa Maziwa yenyewe(galactorrhea);

1. Kutokwa na maziwa kwenye chuchu mara kwa mara wakati hunyonyeshi wala huna mimba

2. Maziwa kutoka baada ya kukamua chuchu au kutoka yenyewe hata ukiwa hujafanya chochote

3. Kutokwa na maziwa yanayohusisha mirija mingi ya maziwa(multiple milk ducts)

4. Hali hii ya kutokwa na maziwa kwenye chuchu huweza kuhusisha titi moja au yote mawili

5. Kutokea kwa mabadiliko ya hedhi, au kukosa kabsa period

6. Kupata maumivu ya kichwa au matatizo ya kutokuona vizuri n.k

Chanzo cha tatizo la Chuchu Kutoa Maziwa yenyewe(galactorrhea)

Tatizo hili la Galactorrhea mara nyingi hutokana na kuwa na kiwango kikubwa sana cha vichocheo aina ya prolactin,

Hii ndyo hormone inayohusika na uzalishaji wa maziwa wakati ukiwa na mtoto.

Hormone ya Prolactin hutengenezwa na pituitary gland, na kazi yake kubwa ni kuhakikisha maziwa yanatoka ili mtoto anyonye,

Hivo basi, unapokuwa na kiwango kikubwa kuliko kawaida cha hormone hii inapelekea kuwa na tatizo la chuchu kutoa maziwa yenyewe ikiwa hata huna mtoto,hunyonyeshi wala huna mimba.

Sababu zingine ambazo huweza kuchangia tatizo la Chuchu Kutoa Maziwa yenyewe(galactorrhea) ni pamoja na;

– Matumizi ya baadhi ya dawa,mfano dawa jamii ya sedatives, antidepressants, antipsychotics pamoja na baadhi ya dawa za presha(high blood pressure drugs).

–  Matumizi ya baadhi ya Vidonge vya mitishamba(Herbal supplements), kama vile Fennel, anise au fenugreek seed

– Matumizi ya Vidonge vya Uzazi wa mpango(Birth control pills)

– Kuwa na uvimbe kwenye tezi ya pituitary au matatizo mengine yanayohusu tezi hii

(A noncancerous pituitary tumor (prolactinoma) or other disorder of the pituitary gland)

– Kuwa na tatizo la tezi aina ya thyroid kutokufanya kazi vizuri(Underactive thyroid (hypothyroidism)

– Kuwa na ugonjwa wa kudumu wa Figo(Chronic kidney disease)

– Matiti kusisimuliwa kupita kiasi(Excessive breast stimulation),

Hii huweza kutokea wakati wa kufanya mapenzi, uchunguzi binafsi wa matiti au msuguano wa muda mrefu unaotokana na nguo uliyovaa.

– Uharibifu wa neva(Nerve damage) kwenye eneo la kifuani, kutokana na sababu mbali mbali kama vile;

  • Upasuaji wa kifua(chest surgery),
  • Kuungua burns
  • Au ajali zingine zozote zinazohusisha kuumia eneo la kifua (chest injuries)

– Kufanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo(Spinal cord surgery), kuumia au kuwa na uvimbe

– Kuwa na msongo wa mawazo(Stress), Watu wengi hawafahamu kuwa Msongo wa mawazo huweza kuchangia mabadiliko mengi mwilini ikiwemo;

  • Hili la chuchu kutoa maziwa yenyewe
  • Kubadilika kwa hedhi n.k
Leo nikufungue Macho kidogo juu ya Tatizo hili.
*Tatizo hili Hutokana na Mvurugiko wa vichocheo vya mwili yaani kitaam Hormone imbalance, Na ifahamike kwamba swala la kutoa maziwa ni mchakato mzima au process ambayo hudhibitiwa na Vichocheo vya mwili yaani Hormones Kama vile Oxcytocin n.k*  Kujua MATATIZO YOTE ambayo yanaweza kusumbua Titi lako.

Tatizo la kutokwa na Maziwa au Maji maji kwenye titi au chuchu, huwapata wanawake wengi na kwa mujibu wa takwimu huonyesha kwamba tatizo hili huathiri asilimia tano hadi 32 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa.Lakini pia tatizo hili mbali na kuwapata zaidi wanawake, huweza kuwatokea wanaume wenye umri Mkubwa, vijana walio katika umri wa balehe, wa kike na wa kiume, watoto wachanga wa kike na wa kiume pia.

Chanzo cha tatizo hili ni nini?

Mvurugiko wa vichocheo vya mwili au baadhi ya homoni mwilini kitaalam kama HORMONE IMBALANCE ndyo chanzo kikubwa cha Tatizo hili

Homoni zinazohusika zaidi na tatizo hili ni homoni ya ‘prolactine’. Vilevile katika hali hii ya kutokwa na Maziwa au majimaji asilimia 50 ya matatizo chanzo chake bado hakijulikani

Kuna matumizi ya dawa kama Methyldopa, madawa ya kulevya na dawa za magonjwa ya akili zote hizi huweza kuchangia hali hii.

Tafiti zinaonyesha,Pamoja na matatizo katika mfumo wa homoni, hali ya kusuguasugua kifua mara kwa mara, hali ya kuwa na hofu  na wasiwasi au shauku f’lani, mfano ya kuhitaji kupata ujauzito husababisha kuamsha homoni za uzalishaji wa maziwa au hayo majimaji.

Vyanzo vingine ni matatizo kichwani kwenye tezi ya ‘pituitary au pituitary adenoma’.
Dawa nyingine zinazoamsha tatizo hili ni kama vile ‘Cimetidine’ ambazo hutibu vidonda vya tumbo.
Pia zipo dawa nyingine za asili ambazo hazijafanyiwa utafiti wa kutosha zinazoweza kusababisha tatizo hili.

Soma: Tatizo la Hormone Imbalance,chanzo,dalili na Tiba yake

Dalili za tatizo hili ni zipi?

Mwanamke mwenye tatizo hili la kutokwa na maziwa kwenye matiti wakati si mjamzito na wala hana historia ya kuwa na mimba, huwa hapati ujauzito.

Mwanaume mwenye tatizo hili hupungukiwa na nguvu za kiume, uzalishaji wa mbegu za kiume huwa mdogo.

MADHARA YA TATIZO HILI

Kwa ujumla tatizo hili husababisha ugumba.
Kwa vijana na watoto wa kiume au wa kike ni vema uchunguzi wa kina ufanyike.
Maziwa yanaweza kutoka tu yenyewe au kwa kuminyaminya matiti au chuchu.

Uchunguzi

Hufanyika hospitalini kwa madaktari wa masuala ya uzazi. Vipimo vya damu kuangalia homoni, matatizo katika matiti, na ikibidi CT-Scan vitafanyika kuangalia matatizo katika tezi ya Pituitary.
Ushauri Wahi hospitali kwani athari ya tatizo hili ni kupoteza uwezo wa kuzaa.

Epuka kuchezea chuchu ziwe zako mwenyewe au za mpenzi wako au za mtoto kwani unaamsha homoni ambazo katika wakati huo hazitakiwi

TIBA

Kwahyo basi ni vizuri kama Umepatwa na Tatizo kama hili,usiache kufikiri mambo mengi,Nenda kutakana na wataalam wa afya kwa Ajili ya kupata Tiba.
KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584 MDA WOWOTE

YOU MUST READ(IMPORTANT)

Magonjwa2 months ago

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani. Watu wengi huweza kupata maumivu chini ya kitovu, lakini umewahi kujiuliza...

Magonjwa3 months ago

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamu

Kaswende ni ugonjwa gani, Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana....

Magonjwa3 months ago

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani Koo kukauka kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa...

Magonjwa3 months ago

Amiba ni ugonjwa gani,Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Amebiasis

Amiba ni ugonjwa gani Wengi wamezoea kusema hivo ila Amiba(amoeba) ni vimelea vyinavyosababisha ugonjwa, na Ugonjwa huo kitaalam ndyo hujulikana...

Magonjwa4 months ago

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba kuwashwa nyayo za miguu; zipo sababu nyingi ambazo huchangia shida...

magonjwa ya wanawake5 months ago

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) Pid ni ugonjwa gani? PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi...

Magonjwa2 years ago

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE) Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto...

Magonjwa3 years ago

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus) tatizo la masikio kupiga kelele Tinnitus, ni Tatizo la masikio kupiga kelele,...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO)

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)

Tatizo la Uke Kujamba TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?) Moja ya vitu...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 FANGASI • • • • • DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE Mashambulizi ya Fangasi sehemu za siri...

Magonjwa3 years ago

CHANZO CHA TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 years ago

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

KUVIMBA MASHAVU YA UKE • • • • • • Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu za kuvimba mashavu...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia)

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia) Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama...

MAGONJWA MBALI MBALI

Magonjwa7 hours ago

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri Yapo magonjwa mbali mbali ya ngozi ambayo huweza kuathiri Sehemu za Siri za Mwanaume...

Magonjwa4 days ago

Dalili za acid reflux,Soma hapa Kufahamu

Dalili za acid reflux: Tatizo la Gastroesophageal reflux disease (GERD), ni tatizo ambalo huwapata Watu wengi,Tatizo hili hujulikana kwa jina...

Magonjwa3 weeks ago

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO Vitiligo ni ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe au ni ugonjwa ambao huhusisha ngozi kupoteza rangi...

Magonjwa3 weeks ago

Mlipuko wa ugonjwa wa macho,Macho Mekundu

Mlipuko wa ugonjwa wa macho,Macho Mekundu Baada ya Ugonjwa huu wa macho kusumbua watu wengi kwa kipindi cha Hivi Karibuni,...

Magonjwa3 weeks ago

Scabies ni ugonjwa gani? Soma hapa kufahamu

Scabies ni ugonjwa gani? Soma hapa kufahamu Utangulizi: Scabies huhusisha mtu kuwa na vipele na muwasho kwenye ngozi yake ambapo...

Magonjwa4 weeks ago

Dalili za ugonjwa wa gono kwa mwanaume

Dalili za ugonjwa wa gono kwa mwanaume Gono ni neno maarufu ambalo kirefu chake ni Gonorrhea na kiswahili chake ni...

Magonjwa4 weeks ago

Dalili Mpya za ukimwi kwenye ngozi

Zipi ni Dalili za ukimwi kwenye ngozi Zipi ni dalili za Ukimwi kwenye ngozi ya mtu? Fahamu hapa kupitia makala...

Magonjwa1 month ago

Madhara ya COVID-19: Athari za Ugonjwa, Asili na Matibabu

Madhara ya COVID-19: Athari za Ugonjwa, Asili na Matibabu Huu ni ugonjwa wa kuambukiza uliosababishwa na kirusi cha corona, ambao...

Magonjwa1 month ago

Ishara za Maambukizi ya Njia ya Mkojo (UTI) kwa Wanaume na Wanawake

Ishara za Maambukizi ya Njia ya Mkojo (UTI) kwa Wanaume na Wanawake Karibu! Hapa kwa makala yenye taarifa muhimu kuhusu...

Magonjwa1 month ago

Vyanzo Vya Kifo cha Ghafla: Sababu Zinazotisha na Jinsi ya Kujikinga

“Vyanzo Vya Kifo cha Ghafla: Sababu Zinazotisha na Jinsi ya Kujikinga” Kifo cha ghafla ni janga lisilotarajiwa ambalo linaweza kumpata...

Trending