Idadi ya watu waliofariki kufuatia mafuriko KENYA imeongezeka hadi kufikia watu 228

#PICHA:Wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya wakiwa katika harakati za uokoaji kufuatia mafuriko.

MAMLAKA nchini Kenya zimesema kuwa idadi ya watu waliofariki kufuatia mafuriko imeongezeka hadi kufikia watu 228.

Tangu siku ya Jumamosi, watu tisa wameripotiwa kufariki huku jumla ya wengine 223,198 wakiathirika na mafuriko hayo. Hata hivyo serikali imetangaza mipango ya kupunguza athari za mafuriko hayo.

Aidha, Msemaji wa serikali ya Kenya, Isaac Mwaura amesema tayari amewahamisha watu 163,000 na kuwapeleka katika maeneo salama.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, tangu mwezi Machi, mvua kubwa na mafuriko vimesababisha uharibifu mkubwa katika nchini za Kenya, Tanzania, Burundi, Somalia, Rwanda na maeneo mengine ya Afika Mashariki.

DW

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!