Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu

Haya ni maneno ambayo umekuwa ukiyasikia sana linapokuja swala la vipimo cha UKIMWI, je unaelewa maana yake?

Nini maana ya HIV negative?

Linapokuja swala la kutafsiri majibu ya kipimo cha HIV yapo maneno mbali mbali ambayo hutumika kama njia ya kuelezea maana ya Majibu yako, Mfano wa maneno ni pamoja na;

Katika Makala hii tumeelezea kuhusu maana ya HIV negative pekee,

Maana ya HIV negative; Tafsiri yake ni kwamba kwa wakati huo uliopima kipimo hakijaonyesha maambukizi yoyote ya VVU.

kwa maana nyingine,Kipimo chako kimeonyesha Hauna maambukizi kwa wakati unaopima.

Lakini Fahamu kwanza Vitu hivi; Majibu kuwa Negative wakati huo unaopima haikuhakikishii kwamba tayari huna maambukizi yoyote ya VVU. Maana kuna kitu kinaitwa “window Period”

window period — Ni muda kati ya kuambukizwa VVU na wakati kipimo chako kinaweza kugundua VVU katika mwili wako.

(the time between HIV exposure and when a test can detect HIV in your body).

Kama bado mwili wako haujatengeneza HIV-Antibodies hata kama una maambukizi kipimo chako hakitaonyesha,kitakupa majibu NEGATIVE.

#SOMA Zaidi hapa kuhusu Window period, 

Ikiwa umefanya kipimo cha HIV baada ya kuwa kwenye mazingira hatarishi na majibu yako yakaja negative, Unatakiwa kupima tena baada ya window period ili kuangalia majibu yako.

Ndyo maana hospital wakikupima,wanakuambia urudi kupima tena baada ya Muda flani.Mfano; mwezi,miezi 3 n.k.

Kama umepima tena baada ya window period,  na hukuwa kwenye Mazingira ya kuambukizwa tena kwa kipindi hiki, na majibu yako yakawa NEGATIVE, Hii ina maana sasa hauna MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI(VVU).

FAQS: Ikiwa nina matokeo hasi, je, hiyo inamaanisha kuwa mpenzi wangu hana VVU pia?

Hapana. Matokeo ya kipimo chako cha VVU yanaonyesha hali yako ya VVU pekee.

Kupima VVU sio njia Pekee ya kujua kama mpenzi wako ana VVU au hana kwa wakati huo.

#SOMA Zaidi hapa,umefanya vipimo wakati huu yupo NEGATIVE ila baada ya muda unashangaa yupo POSITIVE.

Review Article:

https://www.cdc.gov/hiv/basics/hiv-testing/negative-hiv-results.html#:~:text=Skip%20directly%20to,USA.gov

#SOMA HAPA; Jinsi ya Kusoma kipimo chako cha UKIMWI

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!